Monday, May 11, 2015

TFF YATHIBITISHA MICHUANO YA KAGAME ( KAGAME CUP) KUTIMUA VUMBI NCHINI TANZANIA KUANZIA JULAI 11,2015.

Share it Please
SHIRIKISHO la Soka Nchini Tanzania (TFF), limethibitisha rasmi kuwa wenyeji wa  michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati(cecafa), maarufu kama Kombe la Kagame.

Akithibitisha taarifa hiyo, afsa habari wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF)  BARAKA KIZUGUTO amesema taarifa rasmi ya tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa michuano hiyo imetolewa rasmi jumapili ya tar 10/05/2015 makao makuu ya shirikisho hilo baada ya kuombwa na CECAFA.

Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA ambao ndio waandaaji  wa mashindano haya watatoa mialiko kwa klabu zenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya klabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.
Michuano hii inatarajiwa kuanza kufanyika nchini Tanzania kuanzia Julai 11 hadi Agosti 2, mwaka 2015 ambapo inadhaminiwa na raisi wa rwanda mh Paul Kagame.

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author