Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa EAC, Dk Jakaya M. Kikwete.
Wizara ya Mambo ya nje nchini Tanzania imetoa taarifa juu ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili hii ya tar 31/05/2015 ili kuangalia kwa mara nyingine tena hali ya amani nchini Burundi.
Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika karibuni haujaweka wazi kama Raisi wa Burundi aliyejaribiwa kupinduliwa kijeshi wiki mbili zilizopita atakuwepo ila umeweka bayana kuwa Burundi itawakilishwa vyema.
Taarifa za kikao hicho zilitolewa rasmi juzi mei 25 kupitia kwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Mh Bernard Membe ambapo alisema mkutano huo utatanguliwa na kikao cha mawaziri wa wizara za mambo ya nje wa nchi hizo za afrika mashariki.
Wakati huo huo, Upinzani nao nchini humo umegoma kufanya mazungumzo baada ya mmoja wa viongozi wake kuuwawa siku ya Jumamosi.
Machafuko ya kisiasa nchini Burundi yamesababisha zaidi ya Raia 100,000 wa nchi hiyo kukimbilia nchi za jirani Rwanda, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
No comments:
Post a Comment