Sunday, May 3, 2015

MKALI MYWETHER AENDELEZA UBABE MBELE YA PACQUIAO

Share it Please
Utata wa kuwa nani ni mbabe kati ya bondia mmarekani floyd myweather "money" na bondia mfilipino Manny Pacquiao umemalizwa rasmi alfajiri ya leo kwa pambano kali lililohitimishwa kwa ushindi wa bondia floyd myweather dhidi ya mwenzake manny pacquiao.


Awali ya yote pambano hilo lilitawaliwa na tambo za wapambe kutoka pande zote ambapo kila upande uliamini kuwa ni mbabe kuliko mwenzake... tambo hizo ziliitimishwa kwa ushindi wa tofauti ya pointi sita (6) zilizomfanya bondia floyd myweather kuendelea kushikilia rekodi yake ya kutopigwa "UNDEFEATED" kwenye mapambano ya kulipwa ya ndondi.








SCORE CARD KUONYESHA MATOKEO YA KILA ROUND.
Hatimaye matokeo ya ushindi mwembamba wa tofauti ya point sita kutoka kwa majaji watatu walioongoza pambano hilo ulitosha kumtawaza bondia floyd mywether kuwa bingwa wa pambano hilo na hivyo kuendelea kutunza rekodi yake ya kutopigwa tangu kuanza ngumi za kulipwa.

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author