Tuesday, May 12, 2015

MAAFA ZAIDI! IDADI YA WALIOKUFA KWA MAFURIKO DAR YAONGEZEKA.

Share it Please
Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini tanzania kwa ujumla hasa Dar Es Salaam imeongezeka na sasa imefikia watu 10. akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana,kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya D ar es salaam suleiman kova,amesema kuwa kati ya watu hao mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35-38, mwili wake ulipoolewa baada ya kuzama kwenye tope katika mto Msimbazi, Magomeni. Alisema mwili huo wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

 Kamanda aliyataja majina ya watu wengine waliofariki dunia kuwa ni Valerians Eradius (13) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kigogo ambaye alikufa Mei 10 mwaka huu baada ya kuangukiwa na ukuta. Mwingine ni Gervas Shayo (28) mkazi wa Mbezi juu ambaye alikufa maji Mei 8 mwaka huu pamoja na mwanamke mmoja anayekadriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 ambaye jina lake halikufahamika ambaye alikutwa katika bonde la Mkwajuni akiwa amefariki dunia. “Uzoefu unaonyesha kuwa jinsi maji yanavyoendelea kupungua kutokana na kupungua kwa mvua ndivyo madhara yanaonekana. “Ninawaomba wananchi waendelee kutoa taarifa mapema wanapoona mwili wa mtu aliyekufa ili hatua zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na kuiondoa miili ya watu watakaokuwa wamekufa kutokana na athari za mvua inayoendelea kunyesha Dar es Salaam,” alisema Kova.

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author