Friday, May 29, 2015

MAANDALIZI YA LOWASSA KUTANGAZA NIA ARUSHA YAKAMILIKA.


muonekano wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid baada ya maandalizi.
Jiji la Arusha na viunga vyake limeendelea kupokea na kufurika wageni mbali mbali kutoka sehemu tofauti Tanzania wanaotarajiwa kuhudhuria kwenye mkutano mkubwa ambapo aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mbunge wa Monduli kwa tiketi ya chama cha mapinduzi mh Edward Ngoyai Lowassa anatarajiwa kutangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya uraisi kwa tiketi ya CCM kweye uchaguzi mkuu utkaofanyika mapema oktoba 25 mwaka huu.


Baadhi ya wadau wa team lowassa wakiwa ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid kukamilisha maandalizi ya mkutano huo.


gari ikipita mtaani kutangaza mkutano huo.


moja ya majukwaa yatakayotumika.


team Lowassa ndani ya t shirts.
Mapema siku chache zilizopita,kwenye kikao chake na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika nyumbani kwake mjini Dodoma, mh Lowassa aliahidi kutangaza nia yake ya kugombea nafasi hiyo jumamosi hii katika viwanja hivyo vya sheikh amri abeid.
Continue Reading...

MAALIM SEIF KUGOMBEA URAISI TENA ZANZIBAR.


Maalim Seif akipokea fomu ya kugombea urais

Makamu wa kwanza wa raisi wa serikali ya mapinduzi zanzibar na katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, leo amechukua  rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi ya raisi wa serikkali ya mapinduzi zanzibar kupitia chama cha wananchi (CUF).

Maalim seif akitia saini kuthibitisha kuchukua fomu.


Maalim seif akionyesha fomu kwa wananchi na waandishi wa habari.

Maalim seif anakuwa ni mgombea wa kwanza kuchkua fomu ya kuwania nafasi hiyo kupitia chama cha wanachi CUF ambapo historia inaonyesha kuwa amekuwa akikosa wapinzani kwa nafasi hiyo ndani ya chama chake, Maalim Seif anagombea nafasi hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Continue Reading...

Wednesday, May 27, 2015





Continue Reading...

CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT) KUFANYA UCHAGUZI WAKE KITAIFA KESHO MJINI ARUSHA.

Chama cha walimu nchini tanzania (CWT) kinatarajia kufanya uchaguzi wake kesho mjini arusha ili kupata viongozi wa kitaifa wa chama hicho watakaoongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka  mitano.
Tayari mkutano mkuu wa chama hicho umefunguliwa leo jijini arusha katika hoteli ya Ngurdoto kwa hotuba ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk, Jakaya M. Kikwete ambapo ameahidi kutatua changamoto zinazowakumba walimu kabla ya kuondoka madarakani oktoba mwaka huu.

Raisi kikwete akiwasili ukumbini kufungua mkutano huo.
kjj1
raisi kikwete akihutubia walimu wakati wa  ufunguzi wa mkutano huo.

Jumla ya walimu zaidi ya 1000 kutoka sehemeu mbalimbali Tanzania wametarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambapo katika uchaguzi huo walimu wanatarajia kuchagua viongozi katika ngazi za Mwenyekiti, katibu naibu katibu na mhazini.
mr2
Rais kikwete akiteta jambo na mmoja wa waasisi wa chama cha walimu tanzania (CWT) ndugu Thom abieko
Continue Reading...

RAIS OBAMA KUPATA MKWE KENYA ?.... WAKILI KUTOKA KENYA ATANGAZA NIA KUMCHUMBIA MTOTO WAKE.

obama akiwa na mtoto wake wa kike, malia obama
Habari kubwa iliyotawala tasnia ya habari duniani leo ni kuhusu Wakili kutoka nchini kenya Felix kiprono amabye ameushangaza umma baada ya kutangaza nia yake ya kutoa posa ili kumuoa mtoto wa raisi wa marekani,malia Obama mwenye umri wa miaka 16.
Taarifa zinasema kuwa wakili huyo wa kenya amesema yuko tayari kutoa mahari kwa mtoto wa raisi wa Marekani na atatoa ng'ombe 50,kondoo 70 na mbuzi 30 kwa ajili ya mahari ya mtoto wa Obama,Malia Obama.
felix kiprono,wakili aliyetangaza nia kumuoa mtoto wa obama, Malia obama.

Felix amesema anajiandaa kuzungumzia swala hilo na baba wa mtoto huyo atakapo tembelea Kenya ,mwezi Julai. Rais Obama atakuwa na ziara ya kikazi nchini kenya ambapo atatua nchini humo tar 25 ya mwezi wa saba(july) na kuhutubia kwenye mkutano wa dunia kuhusu ujasiriamali, mkutano unaotarajiwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kutoka duniani kote,

Continue Reading...

TAFITI YAMPA USHINDI LOWASSA URAIS 2015.


Nyota ya Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, imeendelea kung’aa baada ya Taasisi ya Samunge Social Sciences Research Center (SSSRC), kufanya utafiti na kubaini kuwa kiongozi huyo ni chaguo la kwanza kwa wananchi.
Utafiti huo uliofanywa miaka miwili kuanzia 2013 hadi 2015, unaonyesha Lowassa anaongoza kwa asilimia 20.7 dhidi  ya wagombea 31.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti Mkuu wa SSSRC, George Nyaronga, alisema utafiti huo waliufanya kwa kutumia madodoso pamoja na mahojiano kwenye mikoa 18.
Utafiti huo na asilimia walizopata wanasiasa wengine kwenye mabano ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema, Dk. Willbrod Slaa asilimia 11.7; Waziri wa Ujenzi, John Magufuli (7.6); Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (7); Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (4.8); Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (4.2)  na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 3.4 sawa na Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (2.4) na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia (1.2).
Alisema pia utafiti huo ulionyesha kuwa Lowassa pekee ndiye anayekubalika na wapiga kura wengi, karibia idadi sawa ya jinsia zote mbili, wanaume 50 na wanawake 49.
Kwa ujumla, Lowassa na vinara wengine 10 wanaotajwa kuwania urais walipata asilimia 67.2, huku asilimia zilizobaki (32.8) zikitwaliwa na wagombea wengine 10 kati ya 20 waliohusishwa katika utafiti huo.
Aidha, Nyaronga alisema hawakuwa na dodoso  linaloorodhesha majina ya wanaopendekezwa kuwa Rais ila majina yalitajwa na wajaza madodoso wenyewe kisha wao wakajaza majina kwenye SSSRC.
Kwa mujibu wa dodoso lenye kichwa cha habari cha katika tafiti kuhusu uchaguzi wa mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kuwa Watanzania wanamtaka mtu mwenye kufanya maamuzi magumu.
Aidha, Nyaronga alisema hawakuwa na dodoso  linaloorodhesha majina ya wanaopendekezwa kuwa Rais ila majina yalitajwa na wajaza madodoso wenyewe kisha wao wakajaza majina kwenye SSSRC.
Kwa mujibu wa dodoso lenye kichwa cha habari cha katika tafiti kuhusu uchaguzi wa mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kuwa Watanzania wanamtaka mtu mwenye kufanya maamuzi magumu.
Alisema kwa maoni ya wengi waliohojiwa na kujaza dodoso, wanaonyesha kuwa Lowassa anakubalika zaidi na kwamba ulifanywa katika mikoa 18 ya Bara na Visiwani, watu 1,000 walijaza dodoso na 6,000 walifanyawa mahojiano.
Alisema utafiti huo uliofanywa kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Morogoro, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Mbeya, Katavi, Kigoma, Tabora, Arusha, Moshi, Iringa, Njombe, Songea, Lindi na Mtwara .
Nyaronga alisema baadhi ya mambo ambayo tafiti hiyo ilikuwa ikitafuta majibu ni masuala yanayohusu changamoto kwa Tanzania kwa sasa, sifa za kiongozi anayehitajika kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la Rais atakayesimamia vizuri changamoto hizo, chama chenye uwezo wa kutupatia rais ajaye kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 na kama Watanzania watapiga kura. 
VYAMA VYA SIASA
Alisema utafiti huo umebaini CCM ina asilimia 53.5 ya kutoa Rais , Chadema yenye asilimia 34.2.
Alisema  vijana wa miaka kati ya 18-25 ambao ni sawa na asilimia 46 wanamtaka Lowassa kuwa Rais, ikifuatiwa na vijana wa miaka 26-30, na  vijana wa kati ya miaka 30-35.
Aliongeza kuwa CCM kina wanachama wengi wenye umri mdogo ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa Tanzania na Chadema ndicho kinachofuatia kwa kupendwa na umri wa miaka kati ya 18 -25.
Mtafiti huyo alisema CCM inapendwa zaidi na watu wenye aina mbalimbali za elimu kuanzia shahada ina watu 144, sekondari ina watu 84  na hata katika elimu ya msingi ina watu 18, ikifuatiwa na Chadema.
Alizitaja changamoto kuu 16 zilizopo Tanzania kwa sasa kama zilivyoorodheshwa na wananchi ambapo wanamtaka Rais ajaye azishugulikie ni elimu, afya, viwanda, ajira, kilimo, miundombinu hafifu, kukosekana kwa utawala bora, uchumi hafifu, nishati, migogoro ya ardhi, mikataba mibovu.
Nyingine ni ukwepaji kodi, rushwa, ufisadi, ubinafsi na kutokuwa na uzalendo.
“Katika tafiti hii tumegundua kuwa Lowassa anaongoza katika kila nyanja kama Rais pendekezwa kuwa Rais wa Tanzania 2015, ukiangalia jinsia zote wa kiume na wa kike wanamtaka Lowassa kuwa Rais,” alifafanua na kuongeza:
“Tafiti hii inaipa chama dira na mwelekeo wa kujua kwamba ni Mtanzania gani ndani ya chama anayehitajika na Watanzania, chama kikishajua hilo hakifanyi kosa kumwacha mtu huyo anayehitajika na Watanzania ili kwanza kukiokoa chama kupoteza dola lakini pia kukilinda kiweze kubaki madarakani.” 
Aliasema chama mbadala wa CCM ni Chadema, takwimu zinaonyesha kuwa, iwapo Lowassa hatapeperusha bendera ya CCM 2015, basi anayetakwa na wananchi kuwa Rais mbadala ni Dk. Willibrod Slaa.
Alisema Machi 2015, taasisi isiyo ya kiserikali ya Positive Thinkers Tanzania ripoti yake ya utafiti  ilioji watu 3,298 na Lowassa alipata watu 752 katika mikoa 13 Tanzania Bara na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,Tibatizibwa Yabutinga, alielezea kuwa Lowassa ni mwanasiasa anayekubalika sana kuwa rais ajaye 2015.
 Alisema katika ripoti hiyo ili orodhesha matokeo yake kuwa Lowassa alipata asilimia 22.8, Slaa  19.5 asilimia ,  Nchemba 10.6, Profesa Lipumba 8.9, John Magufuli 6.8 , Kabwe 6.7, Membe 5.9, Pinda 3.2 ,  makamba 1.6,  Mwandosya 1.2.
Alisema Twaweza sauti za Wananchi, Nov.2014 Imegundua kuwa katika watu 1,445 walioshiriki utafiti ni kuwa wengi wao walisema kuwa changamoto kuu ni Uchumi, elimu na afya na wanasiasa wengi hawatimizi ahadi zao.
Twaweza pia wametoa tafiti kuwa CCM bado kinapendwa na Watanzania kwa asilimia 51 kwa nafasi ya urais, asilimia 46 kwa nafasi ya ubunge na kwa asilimia 47 kwa nafasi za udiwani ikifuatiwa na Chadema.
Alisema ripoti hiyo  ya Twaweza pia inatoa ripoti kuwa vijana chini ya miaka 34, watu chini ya miaka 50 na wazee zaidi ya miaka 50 kwa pamoja wengi wana sapoti kubwa kwa chama cha mapinduzi, na katika nafasi ya urais 2015, ripoti ya Twaweza inasema kuwa ndani ya CCM, kura za wagombea urais kwa tiketi ya CCM ni  Lowassa anaongoza kwa asilimia 17, Pinda asilimia 14, Magufuli asilimia tano, Samuel Sitta asilimia tano, Membe asilimia saba.
Alisema ripoti hiyo ya Twaweza pia iliweka wazi kuwa iwapo uchaguzi utafanywa , basi CCM itaongoza kwa asilimia 47, Ukawa kwa asilimia 28 na kama mtu atasimama binafsi, basi atapata asilimia 19. 
CHANZO: NIPASHE
Continue Reading...

Tuesday, May 26, 2015

MARAIS WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUKUTANA TENA MWISHO WA JUMA HILI KUZUNGUMZIA MGOGORO WA BURUNDI.

Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa EAC, Dk Jakaya M. Kikwete.
Wizara ya Mambo ya nje nchini Tanzania imetoa taarifa juu ya kuwepo kwa mkutano wa Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili hii ya tar 31/05/2015 ili kuangalia kwa mara nyingine tena hali ya amani nchini Burundi.
Mkutano huu unaotarajiwa kufanyika karibuni haujaweka wazi kama Raisi wa Burundi aliyejaribiwa kupinduliwa kijeshi wiki mbili zilizopita  atakuwepo ila umeweka bayana kuwa Burundi itawakilishwa vyema.
Taarifa za kikao hicho zilitolewa rasmi juzi mei 25 kupitia kwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Mh Bernard Membe ambapo alisema mkutano huo utatanguliwa na kikao cha mawaziri wa wizara za mambo ya nje wa nchi hizo za afrika mashariki.
Wakati huo huo, Upinzani nao nchini humo umegoma kufanya mazungumzo baada ya mmoja wa viongozi wake kuuwawa siku ya Jumamosi.
Machafuko ya kisiasa nchini Burundi yamesababisha zaidi ya Raia 100,000 wa nchi hiyo kukimbilia nchi za jirani Rwanda, Tanzania na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Continue Reading...

SAFARI YA MATUMAINI KUANZIA ARUSHA JUMAMOSI HII TAR 30/05/2015

Jumamosi hii ya tarehe 30/05/2015, Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa atazungumza na watanzania kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Arusha kuanzia saa nane mchana. Hii ni katika kuelekea KUANZA kwa ile anayooita "safari ya matumaini"  ambapo anatarajiwa kutangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya uraisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM).
Mh Lowassa aliyasema hayo juzi kwenye kikao chake na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika nyumbani kwake Dodoma ambapo aliongelea mambo mbali mbali ikiwemo afya yake,sakata la richmond, utajiri wake na pia hali ya kisiasa nchi Tanzania kwa sasa. Katika kikao hicho mh Lowassa alitoa ufafanuzi wa mambo hayo ikiwemo kukaa kwake kimya kwa takribani miaka 7 kwenye nyanja ya siasa na kuahidi kutangaza rasmi azma yake ya kugombea nafasi hiyo nyeti na kubwa kwa taifa siku ya jumamosi ya tarehe 30/05/2015 katika viwanja vya Sheikh Amri abeid Arusha.
Continue Reading...

XAVI KUAGWA RASMI BACELONA JUMAMOSI.

Wachezaji wa klabu ya Barcelona watavalia jezi maalum katika mechi yao ya mwisho msimu huu ili kutoa heshima kwa kiungo wao wa kati Xavi ambaye anakamilisha uhusiano wake wa miaka 24 na klabu hiyo . Mchezaji huyo amejiunga na klabu hiyo tangu mwaka 1991 na amefanikiwa kuipa klabu hiyo jumla ya mataji 23 yakiwemo 8 ya ligi, 3 ya uefa, na 2 ya klabu bingwa ya dunia ya fifa.
Mchezaji huo atapewa kwaheri maalum katika mechi dhidi ya Deportivo la Coruna itakayochezwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumamosi.
Xavi mwenye umri wa miaka 35 ambaye atajishindia medali yake ya nane ya la liga alitangaza siku ya alhamisi kwamba ataondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu ili kujiunga na kilabu ya Qatar Al Saad.Ambapo amekiri kuwa uamuzi huo umekuwa mgumu kwake.
Continue Reading...

ANCELOTTI NJE REAL MADRID.



Baada ya kuitumikia kablu hiyo kwa misimu miwili mfululizo,hatimaye klabu ya real madrid kupitia kwa rais wake florentino perez jana imesitisha kibarua cha kocha wake.
Kocha huyo raia wa Italia, aliiongoza Madrid kutwaa taji la kombe la Hispania kabla ya kuibebesha miamba hiyo taji la kumi la klabu bingwa barani Ulaya. 
Pamoja na mafanikio hayo aliyoyapata msimu uliopita, mwaka huu haukuwa mzuri kwa vijana hao wa Benabeu baada ya kuambulia patupu kwa kukosa hata kombe moja japokuwa kikosi cha timu hiyo kinatajwa kuwa cha gharama ya juu. Hasira za viongozi wa klabu hiyo ziliongezeka baada ya kutupwa nje na Juventus katika hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya huku wapinzani wao wakubwa Barcelona ikinyakuwa taji la ligi kuu na kutinga fainali ya klabu bingwa na kombe la Hispania. 
Rais wa Madrid Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari kuwa haikuwa rahis kumtema kocha huyo na kuongeza kuwa kocha mpya atateuliwa wiki ijayo. Makocha jurgen kloop na Raphael Benitez wanapewa nafasi kubwa ya kunyakua kiti hicho.
Continue Reading...

Monday, May 25, 2015

TUME YA UCHAGUZI YATOA RASMI RATIBA YA UCHAGUZI MKUU.



Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ratiba rasmi kwa vyama vya Siasa na wananchi wote itakayotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali  unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo  Jaji wa Rufaa (Mst.) Damian Lubuva imesema kuwa kwa Mamlaka waliyopewa kwa mujibu wa vifungu vya 35B(1), (3) (a), 37 (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,  Sura ya 343, shughuli za uchaguzi zinatarajia kuanza hivi karibuni.
Continue Reading...

MKUTANO WA MABENKI YA AKIBA DUNIANI KANDA YA AFRICA (WSBI) KUFANYIKA TANZANIA MEI 27

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa mabenki ya AkibaDuniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia kesho jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mkutano wa mabenki ya Akiba Duniani (WSBI) Kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia kesho jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa benki hiyo, Mystika Ngongi na kushoto ni Mundakweli Kaniki Meneja Mwandamizi wa Mipango Mkakati ya TPB. Mkutano huo utashirikisha zaidi ya washiriki 100 kutoka nchi mbalimbali Afrika na viongozi wa Dunia wa Taasisi hiyo ya WSBI ambapo pia TBP ndio Benki mwenyeji wa mkutano huo.


SOURCE - Issa Michuzi
Continue Reading...

VIFO ZAIDI VYARIPOTIWA KUTOKANA NA JOTO KALI NCHINI INDIA.

Takriban watu 430 wamekufa kutokana na wimbi la joto linalovuma nchini India.
Watafiti wameripoti kiwango cha juu mno cha joto kimefikia nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.Vifo vingi zaidi vimeripotiwa katika majimbo ya kusini ya Telangana na Andhra Pradesh, ambapo watu 140 wamepoteza maisha yao kuanzia jumamosi wimbi hilo la joto lilipotokea.
Mji wa Allahabad ulioko Uttar Pradesh ulisajili vipimo vya nyuzijoto 48C huku wakaazi wa mji mkuu wa India New Delhi ukiwa na  kiwango cha nyuzijoto zaidi ya  45C ambazo hazijawahi kufikiwa kwa miaka minne iliyopita. Katika mji jirani wa haryana shule zilifungwa kutokana na nyuzi joto kuwa juu na kufikia 48C.
Watafiti wameripoti kiwango cha juu mno cha nyuzijoto 48'C katika maeneo mengi nchini humo.
Maafisa wa utawala nchini humo wameanza kampeini ya kuwahamasisha wananchi kukaa majumbani mwao na kuwashauri wanye waji mengi.
Yamkini viwango vya joto vimekuwa juu zaidi katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita lakini vifo vimeanza kuripotiwa mwishoni mwa juma.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246 waliopoteza maisha yao kuanzia juma lililopita.
Jimbo la Andhra Pradesh ndilo lililopoteza watu wengi zaidi ikiwa na jumla ya watu 246
"asilimia kubwa ya wale waliopoteza maisha ni watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50 walioshinda nje ya majumba yao.'' alisema kamishna wa kupambana na majanga katika jimbo la Andhra Pradesh.
Wakfu wa waandishi wa habari wanasema kuwa watu 186 wamefariki katika wilaya 10 za jimbo la Telangana.
Jumla ya watu 58 wameripotiwa kufa kuanzia siku ya jumamosi.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa imesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa hali hiyo ya joto kuendelea kwa siku kadha zijazo.
Wenyeji wameshauriwa kukaa ndani na kunywa maji mengi
Watu wengine kumi walpoteza maisha yao katika jimbo la Magharibi mwa Bengal.
Waendesha teksi ambazo hazina kiyoyozi hawataruhusiwa kuhudumu kwa saa tano katika mji mkuu wa Kolkata. Hii inafuatia vifo vya madereva wawili.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa inasema kuwa hali hiyo ya juu ya joto inatokana na ukosefu wa mvua.

Continue Reading...

KIBONZO CHA MWEZI NA KP.


Continue Reading...

JIANDIKISHE KUPIGA KURA. NI HAKI YAKO!

.
Continue Reading...

URAISI 2015. LOWASSA AFANYA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI.


lowassa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mjini dodoma.

Lowassa akisalimiana na mhariri msaidizi wa gazeti la Jamhuri, Manyerere Jackson.
Lowassa: Sihusiki na Richmond, ilitungwa kunichafua. Sitohama CCM!
Habari za kuaminika kutoka chanzo chetu zinaripoti kuwa Waziri Mkuu aliejiuzulu Edward Lowassa amesafirisha wahariri wakuu wa vyombo vyote vya habari toka Dar es salaam na kufanya nao mkutano maalum leo nyumbani kwake mjini Dodoma. Katika mkutano huo kwa ufupi Lowassa amesema yafuatayo;
1. Amesema Hahusiki lolote na sakata la Richmond na ndio sababu hata kamati ya Mwakyembe haikuona sababu ya kumhoji. Amesisitiza kuwa cheo cha uwaziri mkuu ndio ilikuwa lengo la kamati ya mwakyembe na spika wa bunge kipindi hicho Samwel Sitta. Amesisitiza hicho sio kikwazo kwake katika kuingia Ikulu kwani sakata la Richmond lilipikwa kumchafua. Amechukua muda mrefu kuzungumzia hili la Richmond na amesema atalisema zaidi Arusha wikendi hii.
2. Anaamini kila mtangaza nia ana makundi ya kumuunga mkono. Yeye katika mkutano huu na wahariri leo ameambatana na Nazir Karamagi, Peter serukamba, Diana chilolo, Hussein Bashe na wengineo huku wengi wakiwa ni waliojeruhiwa katika serikali ya awamu ya nne akiwemo Aliekuwa DC Igunga Elibariki Kingu. Pia aliyekuwa mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeti Misoki ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa mahusiano na mawasiliano katika timu ya kampeni ya Lowassa. Amehoji kwani akina Karamagi wana tatizo gani na kwani wao sio binadamu?
3. Lengo kuu atakaloanza nalo ni Elimu na sio Kilimo kwanza cha serikali ya JK. Amesema serikali ya JK ilikosea kuanza na kilimo na kuweka kando elimu. Ametangaza kuwa sera yake ni Elimu Kwanza.
4. Kuhusu pesa anasema anapata michango ya rafiki zake na ataendelea kupokea michango hii wakati wote wa harakati zake na haina madhara yotote.
5. Anasema hatahama CCM na asiyemtaka yeye CCM ndie aondoke ndani ya chama kwani yeye ana uhakika wa kupata nafasi kuwania urais.
6. Amesema hatalipa kisasi kwa lolote lililomtokea katika siasa. Amemwachia Mungu kwani yeye ni mcha Mungu.
7. Amesema Arusha itawaka moto tarehe 30 mwezi huu na kuwataka watanzania kutega sikio kwani ataanika kila jambo kuhusu mustakabali wa nchi hii na mipango yake ya kuiinua nchi kiuchumi katika miaka kumi ijayo.
Hayo ni kwa ufupi. Wahariri wakuu katika media zote kupitia Jukwaa la Wahariri walikuwepo, na Absalom Kibanda (New Habari) na Nevil Meena (Free Media) ndio walikuwa waratibu wakuu wa mkutano huu. Chanzo chetu cha habari kinaendelea kufatilia kwa umakini habari hizo. blogu yako ya habari inaahidi kuendelea kukuhabarisha kwa matukio yote yanayotokea na yatakayotokea kueleka mchakato huu wa uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Continue Reading...

DROGBA AAGA RASMI CHELSEA.




Ikiwa Ligi kuu ya Uingereza imekwisha huku timu ya Chelsea wakiwa mabingwa wa msimu huu, mshambuliaji wa klabu hio Didier Drogba amefanya maamuzi magumu juu ya maisha yake ya soka na klabu hio.
Drogba atawaacha Mashabiki wa Chelsea watakuwa na furaha baada ya kuwa mabingwa lakini wakati huo huo watakuwa na huzuni ya kumpoteza mshambuliaji wao kipenzi Didier Drogba ambaye ametangaza kuiacha klabu hio na kwamba hii ndio mechi yake ya mwisho.
Drogba aliandika ujumbe kupitia account yake ya Instagram kuwa ” Nimezungumza na kocha wangu Jose Mourinho kuhusu hatma yangu kuwa nataka kuendelea kucheza soka hata msimu moja na ili nicheze zaidi soka lazima niende timu nyingine” aliongeza "mashabiki wa klabu hii wanafahamu mapenzi niliyonayo juu ya klabu na natamani kurudi tena hapa siku moja lakini kwa nafasi nyengine".
Drogba anamiaka 37 alijiunga kwa mara ya kwanza na Chelsea mwaka 2004 na kuwepo kwenye klabu hiyo kwa takribani misimu minane yenye mafanikio ambapo ameifungia klabu ya chelsea jumla ya magoli 104  kwenye mechi 253 za ligi. Kwa msimu huu drogba ameifungia klabu hiyo magoli saba (7) tangu kujiunga kwake kwa mkataba mfupi wa mwaka mmoja.
Screenshot_2015-05-24-15-24-10
Continue Reading...

Thursday, May 21, 2015

TO ALL MUSLIMS! WELCOME RAMADHAN CONFERENCE.

Continue Reading...

NEWS! WALEMAVU WAANDAMANA NA KUFUNGA BARABARA DAR!

Kundi la walemavu wajasiriamali kutoka umoja wa wafanya biashara wenye ulemavu dar  (uwawada) leo wamefanya maandamano yaliyopelekea kufunga barabara kadhaa katika mkoaa wa dar wakishinikiza serikali kutoa maelezo juu ya uvunjaji wa meza za biashara katika soko la machinga complex la ilala dar es salaam unaodaiwa kufanywa na askari wa jiji usiku wa kuamkia jana.

Mkusanyiko mkubwa wa wafanyabaishara hao ulionekana maeneo ya ilala kwenye makutano ya barabara ya kawawa na uhuru jirani na zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa dar es salaam ambapo ndipo hasa walitaka uongozi wa mkoa na wilaya ya ilala watoe maelezo juu ya kuvunjwa kwa mabanda yao ya biashara.
baadhi ya walemavu waliokuwa sehemu ya mgomo huo


foleni ya magari iliyosababishwa na mgomo huo.

Baadhi ya walemavu hao wakionekana kufunga pande mbili za makutano ya barabara hizo za Kawawa na Uhuru jijini  Dar Es Salaam. Picha na MichuziBlog.
baadhi ya walemavu wakiwa wamefunga makutano ya barabara ya uhuru na kawawa mapema leo.

Mgomo huo wa walemavu uliodumu kwa masaa matatu ulihitimishwa baada ya mkuu wa wilaya ya ilala mh Raymond Mushi kuahidi kuwa manispaa ya ilala itafanya uchunguzi ili kubaini kama kuna uharibifu uliotokea na kulipa fidia kwa wahanga.
Continue Reading...

Wednesday, May 20, 2015

KIPINDUPINDU CHAIKUMBA KAMBI YA WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI ILIYOPO KIGOMA.


WAKATI hali ya usalama nchini Burundi ikiwa bado tete, wakimbizi 558 walioko katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma wanaugua ugonjwa wa Kipindupindu.
Ugonjwa huo ulilipuka hivi karibuni baada ya wakimbizi hao kuingia nchini wakikimbia machafuko ya kisiasa yanayoendelea nchini humo.
Akizungumza jana, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Steven Kebwe, alisema hadi sasa wakimbizi 15 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Alisema tangu Aprili 24 mwaka huu wakimbizi 2,458 walikuwa wakiharisha na kutapika na sampuli 11 kati ya 13 zilizochukuliwa juzi zilithibitisha kuwa wanaugua ugonjwa wa kipindupindu.
“Tumeshirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na tayari tumepeleka timu ya wataalamu ambao wametembelea maeneo ya Kagunga na Nyarugusu kutathmini na kutoa elimu ya afya kwa umma.
“Tumefanya tathmini katika mikoa ya Kagera, Geita na Katavi ambayo inapakana na Burundi,” alisema Dk. Kebwe.
Alisema wamepeleka dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya dharura pamoja na kuanzisha mfumo wa kufuatilia magonjwa yakiwemo ya mlipuko katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kwa mujibu wa Dk. Kebwe, ugonjwa wa kipindupindu unatokana na kula chakula au kunywa kinywaji chenye vimelea vinavyosababisha kuharisha ambavyo hupatikana kwenye kinyesi, matapishi au majimaji kutoka kwa mgonjwa.
Moja ya vyanzo vya maji kwenye kambi hiyo.
Alizitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni kuharisha mfululizo bila maumivu ya tumbo, kinyesi cha majimaji kinachofanana na maji ya mchele, kutapika mfululizo, kuishiwa nguvu na kwamba ndani ya masaa sita kama hakuna huduma mgonjwa anaweza kupoteza maisha.
Kuhusu gharama za matibabu, alisema wametoa kwenye akiba ya magonjwa ya dharura na mlipuko lakini zitarejeshwa baadaye na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).
Alitoa wito kwa wananchi kuzingatia usafi wa mazingira, usafi wa vyoo, kunywa maji safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kutoka chooni na kusafisha vyakula.

Continue Reading...

TEKNOLOJIA! FAHAMU TOFAUTI KATI YA 2G,3G NA 4G

1G 


ni simu za kizazi cha kwanza kabisa katika teknolojia ya mawasiliano katika mfumo wa bila waya (wireless). Wakati huu ndio simu za mkononi (zikiwa kubwa kwelikweli enzi hizo) zilianza kutengenezwa na kununuliwa. Hii ilikuwa katika miaka ya 1980, na moja ya simu maarufu enzi hizo kuanza ni Motorola DynaTAC. Hakukuwa na huduma ya intaneti katika mfumo huu wa teknolojia. Kulikuwa na modemu kwa ajili ya intaneti kwa ajili ya kutumika kwenye kompyuta, ila zilikuwa zinatumia teknolojia ya 'Dial up', yaani kwenye mipangilio (settings) unakuwa kama unapiga simu hivi ndio unakuwa unaunganishwa katika huduma ya intaneti. Na gharama ilikuwa unalipia kulingana na muda ambao umekuwa umeunganishwa kwenye intaneti, yaani kama vile dakika za maongezi.
Kuja na uwezo wa kujiunga mara zote bila ata ya kutumia teknolojia ya Dial Up ndio kulizaa teknolojia ya 2G kwa kuanzia na GPRS.

Teknolojia za 2G;
GPRS


GPRS ndiyo teknolojia ya kwanza kwenye simu iliyoleta uwezo wa kutumia data, yaani intaneti. Teknolojia hii ipo katika familia ya teknolojia za 2G, yaani '2nd Generation'. Kirefu cha GPRS ni 'General Packet Radio Service', kiasi kikubwa zaidi cha kasi ya intaneti ndani ya teknolojia hii ni hadi kufikia kati ya kb 35 hadi 171 kwa sekunde. Lakini mara nyingi huwa chini ya hapo.Katika kutumia teknolojia hii ndio utaweza kufungua mtandao wowote au ata kutuma barua pepe kwenye simu yako, tatizo ni moja tuu..itachukua muda mrefu sana mtandao kufunguka au ata hiyo barua pepe kwenda.
Hapa mfano wa kasi yake ni kama vile mwendo wa kutembea kwa miguu..

EDGE


Kibongo bongo, yaani Tanzania utakuwa umeona sana alama ya E au EDGE ikiwa imekamilika katika simu yako. Ukiona E, ujue ni EDGE na kirefu chake kimombo ni 'Enhanced Data rates for GSM Evolution). Kwa kiasi kikubwa teknolojia hii ilitengenezwa kama maboresho ya teknolojia ya GPRS, hapa uwezo uliongezwa zaidi katika suala la kasi ya uhamishaji wa data katika huduma ya intaneti.Teknolojia hii huwa inategemewa kuweza kuwa na kasi ya hadi kufikia kb 120 hadi 384 kwa sekunde, lakini mara nyingi huwa chini ya hapo. Teknolojia hii ipo juu zaidi ya GPRS lakini ni ya chini sana ukilinganisha na 3G. Wataalamu wengine huwa wanaiona EDGE kama ni 2.5G au 2.75G kutokana na kuwa kasi zaidi ya GPRS.
Hapa mfano wa kasi yake tunaweza fananisha na kamwendo ka kwenda kwa baiskeli. Unajitahidi kidogo ila si kasi sana.

3G - pia HSPA n.k



Teknolojia ya 3G ilitengenezwa kwa ajili ya kutoa maboresho mapya ukilinganisha na teknolojia nzima ya 2G. Teknolojia hii iliingia sokoni rasmi mwaka 2001, na mitandao mingi ya simu ikaanza kuitumia mara moja katika maeneo yenye ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti. Kuja kwake kulikuwa maarufu sana hadi baadhi ya makampuni ya kutengeneza simu kama vile Apple waliamua kuita baadhi ya simu zao '3G', kuna iPhone 3G na iPhone 3GS zilitoka kipindi hicho, hii yote ni kutaka kufahamika ya kwamba simu hizo zitaweza kupata intaneti ya kasi zaidi.Kasi kubwa zaidi inayoweza kupatikana ndani ya mitandao ya 3G ni hadi kufikia Kb 384 hadi MB 2 kwa sekunde.Je HSPA, HSPA+, EVDO, HSDPA n.k ni nini?
Hizi ni teknolojia za maboresho zaidi ya 3G na zimefanikiwa kukuza kasi ya intaneti ya 3G kufikia hadi zaidi ya MB 100 kwa baadhi yake, kasi hii si kwa watumiaji wadogo kupitia simu kama mimi na wewe. Lakini bado kwa watumiaji wadogo, mimi na wewe kasi inakuwa ndogo,lakini bado utaona utofauti kulinganisha na 3G hasili. Maboresho haya ndiyo yanaleta majina mengine kama vile 3.5G, 3.75G n.k.
Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema apa una mwendokasi wa pikipiki. Ni maendeleo makubwa sana kutoka kwa utumiaji wa basikeli, yaani EDGE.

4G!



Teknolojia ya 4G ina kiwango cha kuwezesha hadi kasi ya intaneti ya GB 1 kwa sekunde kwa maunganisho ya kiwaya, yana 'fiber', na kwa eneo la kimawasiliano ya simu inatakiwa kuwa na kasi ya MB 100 kwa sekunde. Kumbuka mabadiliko makubwa ya kiteknolojia yamefanyika kuwezesha kasi hizi kubwa za intaneti, mfano teknolojia za 2G na 3G zote zilikuwa zinapatikana katika mifumo ya GSM(mitandao yetu mingi inatumia mfumo huu) na CDMA (mfumo unaotumiwa na TTCL), lakini 4G inapatikana katika mifumo mipya ya LTE (Long Term Evolution) na WiMAX.Ingawa kiteknolojia WiMAX inatakiwa kutoa intaneti ya hadi ya kasi ya MB 40 kwa sekunde na LTE hadi kasi ya MB 100 kwa sekunde mara nyingi hali inakuwa tofauti unapokuja kwa watoa huduma za intaneti katika teknolojia hizo. Kiutumiaji wa kawaida tegemea kasi ya kati ya MB 4 hadi MB 30 kwa sekunde, na hii ni kasi kubwa tuu ukilinganisha na kile unachoweza kupata ukiwa unatumia 3G. Kiuhalisia pia ni kwamba ili uweze kufurahia kasi hizi kifaa chako pia kinatakiwa kiwe na uwezo wa kupokea intaneti ya kasi hiyo.
Kwa mfano wa kasi hapa basi tunaweza sema katika teknolojia hii unasafiri kwa ndege, utawahi kufika sana kulinganisha na teknolojia za nyuma.

5G?


Tayari nguvu zimewekwa katika kujenga teknolojia ya 5G ingawa ata hii 4G bado haijaweza kusambaa zaidi kama 3G. Na ni kampuni ya Samsung ndio wamejikita katika kuleta teknolojia wanayofikiria itaweza kuwa hadi mara 100 haraka zaidi ya 4G!
Continue Reading...

Thursday, May 14, 2015

SERIKALI : MADEREVA ENDELEENI NA UTARATIBU WA ZAMANI KUHUISHA LESENI ZENU.

Serekali imesema hakutakuwa na mafunzo ya udereva kwa madereva wa mabasi na malori wala madereva kutakiwa kwenda kusoma kozi fupi ili kuhuisha leseni zao kama ilivyotangaza hapo mwanzo na kusababisha mgomo wa madereva. Kauli hiyo imetangazwa jana na kamanda wa kikosi cha polisi wa barabrani bw Mohammed Mpinga alipokuwa akitangaza uamuzi huo wa serikali.

mwenyekiti wa madereva clemence masanja akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza uamuzi huo mapema jana.

Alisema kuwa madereva wenye madaraja E,C1,C2 na C3 ambao walitakiwa kupitia kozi fupi ya udereva kila baada ya miaka 3 kulingana na kanuni zilizopitishwa mwaka 2014 na mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu (SUMATRA),mamlaka ya mapato tanzania (TRA), chama cha wamiliki wa mabasi (TABOA), Chuo cha usafirishaji (NIT), chama cha wamiliki wa magari ya mizigo (TATOA),vyama vya madereva na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.
Kamanda mpinga alitoa wito kwa madereva kuwa wavumilivu na matatizo yao wakati kamati ya kudumu ya kutatua matatizo katika sekta ya usafirishaji ikiendelea kuyataftia ufumbuzi wa kudumu.
kamanda wa polisi kikosi cha uasalama barabarani mohammed mpinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Continue Reading...

Tuesday, May 12, 2015

MAAFA ZAIDI! IDADI YA WALIOKUFA KWA MAFURIKO DAR YAONGEZEKA.

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini tanzania kwa ujumla hasa Dar Es Salaam imeongezeka na sasa imefikia watu 10. akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana,kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya D ar es salaam suleiman kova,amesema kuwa kati ya watu hao mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 35-38, mwili wake ulipoolewa baada ya kuzama kwenye tope katika mto Msimbazi, Magomeni. Alisema mwili huo wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.

 Kamanda aliyataja majina ya watu wengine waliofariki dunia kuwa ni Valerians Eradius (13) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kigogo ambaye alikufa Mei 10 mwaka huu baada ya kuangukiwa na ukuta. Mwingine ni Gervas Shayo (28) mkazi wa Mbezi juu ambaye alikufa maji Mei 8 mwaka huu pamoja na mwanamke mmoja anayekadriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 na 45 ambaye jina lake halikufahamika ambaye alikutwa katika bonde la Mkwajuni akiwa amefariki dunia. “Uzoefu unaonyesha kuwa jinsi maji yanavyoendelea kupungua kutokana na kupungua kwa mvua ndivyo madhara yanaonekana. “Ninawaomba wananchi waendelee kutoa taarifa mapema wanapoona mwili wa mtu aliyekufa ili hatua zichukuliwe mara moja ikiwa ni pamoja na kuiondoa miili ya watu watakaokuwa wamekufa kutokana na athari za mvua inayoendelea kunyesha Dar es Salaam,” alisema Kova.

Continue Reading...

Followers

Follow The Author