Sunday, June 7, 2015

MH AMINA SALUM ALI, MWANAMKE JASIRI ANAYEUTAKA URAISI TANZANIA 2015.

Share it Please

Mh Balozi amina salum ali wakati wa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na CCM kugombea uraisi wa Tanzania.



Mh Balozi amina salum akizungumza na Raisi Jakaya Kikwete.
Balozi wa kudumu wa nchi za afrika kwenye umoja wa mataifa nchini Marekani, mh Amina Salum Ali juzi ameweka historia katika siasa za chama cha mapinduzi nchini  Tanzania baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake (CCM) kugombea kiti cha uraisi nchini humu akichuana na wanasiasa mashuhuri na viongozi wastaafu wa serikali nchini humu kama mh Edward lowassa( mbunge waziri mkuu mstaafu), Mh Samuel sitta( waziri wa uchukuzi) , mh bernard Membe ,Mh Steven wassira, Mh january makamba na wengine wengi.

Historia yake kwa ufupi.
Amina Salum Ali ni Balozi wa umoja wa nchi za kaifrika nchini Marekani. akiwa Kama balozi mwanamke wa kwanza kuwakilisha Umoja wa Afrika , katika utumishi wake amekuwa na vipaumbele vya ya kutetea haki za wanawake na masuala ya watoto. 
Balozi Amina Salum Ali pia ni mwanzilishi wa mfuko wa maendeleo wa wanawake zanzibar (Zanzibar Women welfare Trust) ambao una lengo la kupambana na matatizo ya afya kwa wanawake na watoto kama VVU / UKIMWI. 
Balozi Amina amekuwa ni Mwanachama wa muda mrefu wa Bunge, ambapo amewahi kushika nafasi mbalimbali za uwaziri katika serikali ya Tanzania, ikiwemo nafasi ya waziri wa nchi katika ofisi ya waziri mkuu wa Zanzibar. 
Balozi Amina Ali pia ni mwanachama wa Benki ya Kiislamu  ya Maendeleo ya Wanawake akiwa mjumbe wa Jopo la Ushauri na aliwahi kuwa mjumbe wa bodi ya taasisi mbalimbali kama vile TTCL na Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro, Tanzania. 
Aidha, balozi Amina ameweza kuanzisha na kusimamisha imara taasisi mbalimbali za kujenga uwezo, ikiwa ni pamoja na Rais Trust Fund kwa ajili ya Kujitegemea. 
Balozi Amina ana shahada ya kwanza katika uchumi na MBA katika masoko.

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author