Wednesday, June 24, 2015

ANASWA UWANJA WA NDEGE AKISAFIRISHA SHEHENA YA MALIASILI.

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNAI), linamshikilia, raia wa Kuwait, Hussein Mansoor, kwa kukutwa na kobe hai 173 aliokuwa akiwasafirisha kueleka nchini kwake.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa JNIA, Clemence Jingu alisema abiria huyo mwenye hati ya kusafiria yenye namba 003870237, alikamatwa usiku wa kuamkia jana akijitayarisha kupanda ndege ya Emirates iliyokuwa ikielekea Kuwait kupitia Dubai.
Jingu alisema raia huyo alikamatwa saa tano usiku katika eneo la abiria wanaoondoka, baada ya polisi wa JNIA kwa kushirikiana na maofisa wa Wizara ya Maliasili kufanya ukaguzi na kugundua kobe hao wakiwa wamefichwa kwenye masanduku makubwa mawili.
“Hii ni moja ya kazi kubwa ambazo tunazifanya kwa sasa hapa JNIA, ila tutahakikisha kuwa hakuna nyara za Serikali zitakazotaifishwa na kupitishwa hapa kwa kuwa tumeimarisha ulinzi maradufu,” alisema Jingu.
Jingu alisema kobe hao wenye thamani ya Sh 30 milioni ni miongoni mwa nyara muhimu za Serikali ambazo zimekuwa zikitaifishwa kupitia mbinu mbalimbali.
“Pamoja na kuimarisha ulinzi, lakini tutahakikisha JNIA inakuwa bora kuliko viwanja vingine vya Afrika Mashariki na zaidi hasa kuhakikisha ulinzi unapewa kipaumbele” alisema.
Kamanda wa Polisi wa JNIA, Khamis Suleiman, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.
Tukio hilo lilithibitishwa pia na Kamishna wa Interpol, Tawi la Tanzania, Gustav Babile ambaye alisema raia huyo alikamatwa na wanyama hao huku akiwa na vibali halali.
Mmoja wa wafanyakazi wa JNIA (jina linahifadhiwa) alisema kabla ya kukamatwa, ilionekana kuna mpango umefanywa ili kumpitisha raia huyo bila kugundulika kwani taa za eneo la ukaguzi zilizimwa kwa saa kadhaa uwanjani hapo.
“Si kawaida taa kuzimwa lakini wakati yeye anapita taa zilizima jambo linaloonyesha kuwa ni njama zilizopangwa lakini hata hivyo hazikufanikiwa,” kilisema chanzo hicho.
Kadhalika chanzo hicho kilisema raia huyo aligunduliwa na askari wa maliasili akiwa tayari ameshapita katika vizuizi vyote vya ukaguzi na ameshaingia katika eneo la abiria wanaoondoka.
Tukio hili linafanana kwa kiasi kikubwa na lile lililotokea Januari 8, mwaka huu, ambapo raia mwingine wa Kuwait, Ahmed Ally Mansour alikamatwa uwanja wa JNIA akiwatorosha kenge hai 149 wenye thamani ya Sh 6.3 milioni.
CHANZO : GAZETI LA MWANANCHI
Continue Reading...

UGUNDUZI ! WANAFUNZI WAVUMBUA KONDOMU INAYOGUNDUA MAAMBUKIZI YA GONJWA ZA ZINAA.


Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.
Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali, 14, Muaz Nawaz, 13 na Chirag Shah, 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex, nchini Uingereza.null
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.

''tuliazimia kumpa onyo mtumiaji wa mipira hii kuwa mpenzi wake yuko salama ama ni mgonjwa bila ya wasiwasi wa kupimwa hospitalini''.
Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .
Daanyall alisema kuwa "Walizindua kondomu hiyo ilikuifaidi kizazi kijacho''
''Kwa hakika swala la usalama wa mpenzi wako ni swala la kibinafsi kwa hivyo ni swala linalopaswa kupewa kipaombele haswa ikifahamika kuwa tunawajibu wa kuchochea ngono salama bila ya kuwashurutisha wapenzi wetu kufika hospitalini bila wao wenyewe kukusudia''

null
Wavumbuzi hao wanasema kuwa hiyo ni mojawepo ya njia salama ya kubaini usalama penzi lenu.

Wanafunzi hao waliwalitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.
Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia, TeenTech, Bwana Maggie Philbin, alisema kuwa
"Ni wajibu wetu kama jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu''

SOURCE: BBC
Continue Reading...

CHARLES MKWASA AMRITHI NOOJ KOCHA TAIFA STARS.

Mkwasa
Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa  ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekizi.
Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.
Continue Reading...

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KAIMU MUFTI MKUU WA TANZANIA IKULU LEO,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila  Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu  na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Continue Reading...

MEDIA CAR WASH FOR CANCER KUSAIDIA WANAHABARI WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA CANCER.

Continue Reading...

ZIJUE FAIDA ZA TENDE MWILINI.


Je unajua kwamba tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamin, protini, wanga na mafuta?. Mbali na utamu wake tende ambazo hulika sana mwezi wa ramadhan zina faida nyingi sana kwa mwili wa binadamu. Zijue faida zake.

Tende ni tunda ambalo linayeyuka kirahisi tumboni na lenye faida nyingi sana ambazo hulifanya liwe tunda la kipee.
Kwa leo tutazielezea baadhi ya faida za tende mwilini:

1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

3- Tende husaidia pia kwenye mambo ya malavi davi. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.
7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.
9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.
10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
Continue Reading...

SHEIKH ABOUBAKAR ZUBER ATEULIWA KUKAIMU NAFASI YA MUFTI TANZANIA.

Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania - Sheikh Abubakar Zuberi
Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania – Sheikh Abubakar Zuberi
Aliyekuwa mmoja wa wajumbe wa baraza kuu la Ulamaa BAKWATA, Sheikh Abubakar Zuberi, ndiye aliyetajwa kushika kwa muda wa siku 90 nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Waislamu Tanzania (MUFTI) kufuatia kifo cha aliyekuwa Mufti Mkuu, Sheikh Idd Shaaban Simba aliyefariki mnamo wiki moja iliyopita, kabla ya uchaguzi utakaofanyika kumpata kiongozi mkuu kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanaotajwa kuweza kushika nafasi hiyo ni pamoja na Kadhi Mkuu, Sheikh Abdallah Mnyasi na Sheikh Ali Muhidin Mkoyogile.
Wengine ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Ferej, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Hamid Masoud Jongo.
Sheikh Abubakar Zuber ametangazwa asubuhi hii ya leo kuwa ndiye mkaimu wa nafasi hiyo ya juu kabisa kiuongozi katika dini ya kiislamu.
Sheikh Zuber atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (siku 90) kuelekea katika uchaguzi wa kumpata atakayerithi nafasi hiyo kwa mamlaka kamili.
Zipo hisia pia kuwa huenda Sheikh Abubakar akapitishwa kuishikilia nafasi hiyo baada ya kipindi hicho kupita endapo kura nyingi zitaelekezwa kwake.
Continue Reading...

Friday, June 19, 2015

#FACT. TRY IT!

It is impossible to sneeze with your eyes open
Continue Reading...

Thursday, June 18, 2015

ALLYKIBA ATEULIWA KUWA BALOZI,VITA DHIDI YA UJANGILI TANZANIA.

WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na asasi za kimataifa WildAid na African Wildlife Foundation na Balozi mpya wa WildAid muimbaji maarufu Ali Kiba, wamezindua kampeni mpya ya kuongeza ufahamu na kuielimisha jamii kuhusu tatizo sugu la ujangili linaloikabili Tanzania. Kampeni hii inatarajiwa kuongeza mwamko wa taasisi za kiraia katika kulinda tembo na wanyama wengine. 
Tanzania imepoteza asilimia 60 ya tembo wake katika miaka sita iliyopita zaidi kutokana na ujangili kwa ajili ya pembe za ndovu. Wanaonufaika zaidi na pembe za ndovu ni baadhi ya wafanyabiashara haramu wa nchini China na katika nchi nyingine zenye watumiaji wa bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu huku Tanzania ikibaki kuwa muathirika wa tatizo hili.

Msanii Ally Kiba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.

“Watalii wengi wanaokuja nchini hupendelea zaidi kuwaona Tembo, na utalii unachangia asilimia 12 ya pato letu la taifa (GDP)”, alisema Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii. “Tembo wetu ni utajiri mkubwa kwa nchi yetu katika njia mbalimbali na serikali yetu imedhamiria kukomesha uhalifu huu. Hata hivyo hatuwezi kufanya jambo hili peke yetu, tunahitaji kupata msaada wa wananchi wote katika jitihada zetu katika kukomesha wizi huu wa urithi wa taifa letu”.

Muimbaji huyo maarufu wa Afrika Mashariki Alikiba ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa kampeni hii alisema. “Ninafurahi kupewa heshima hii na nitatumia nafasi hii kutoa kila mchango ninaoweza kutoa katika jitihada hizi za kulinda wanyama pori wetu”, alisema Ali Kiba. “Tembo wetu wazuri lazima waachwe waweze kuishi katika mazingira yao ya asili badala ya kuishia kuwa pambo kwenye meza ya mtu”, aliongeza Ali Kiba.Katika utafiti wa hivi karibuni uliohusisha zaidi ya Watanzania 2,000 waishio vijijini na mijini, zaidi ya asilimia 79 walioshiriki walisema kuwa watasikitika endapo tembo watatoweka Tanzania na zaidi ya asilimia 73 walisema wanaamini kuwa tembo ni utambulisho na urithi wa taifa.

“Watanzania wote bila kujali wanapoishi, ni wadau wa rasilimali hii ya wanyama pori”, alisema Peter Knights, Mkurugenzi Mtendaji wa WildAid. Kauli mbiu ya kampeni hii ‘Ujangili Unatuumiza Sote’ inatukumbusha kuwa wale wote wanaojihusisha na ujangili wa kuua tembo na kusafirisha pembe za tembo hao kimagendo kwenda Asia ya Mashariki wanatuumiza Watanzania sote”.

Dk. Patrick Bergin, Afisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, alisisitiza kwamba ujangili unachafua jina la Tanzania nchi ambayo ina sifa ya kuwa na hifadhi kubwa ya tembo.“Tanzania imekuwa ikijulikana kwa kuwa na makundi makubwa ya tembo ambapo ukijumlisha na Botswana na Zimbabwe utaona kuwa nchi hizi kwa pamoja zina nusu ya tembo wote waliopo barani Afrika,” alisema Bergin. “Hata hivyo, kiwango cha sasa cha ujangili kinatishia kufuta sifa hii ya kipekee. Wakati Watanzania wanazidi kujifunza zaidi kuhusu janga hili kupitia hii kampeni, tunaamini kuwa watashirikiana na sisi kuilinda mali hii adimu.”  Kampeni hii itatumia redio na televisheni, mitandao ya kijamii, magazeti, mabango na filamu zitakazoonyeshwa maeneo ya wazi ili kuwafikia wananchi wengi iwezekanavyo wakiwemo wakazi wa vijiji vilivyoko ndani ndani. Video mpya inayomhusisha Ali Kiba na Jacqueline Mengi tayari imetengenezwa na imeonyeshwa kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa kampeni hiyo.
Continue Reading...

NGASSA AZUIWA KUCHEZEA TAIFA STARS.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kuicheze timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Uganda Jumamosi.
CAF imeiambia TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwamba Ngassa haruhusiwi tena kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kwa sababu siyo tena mchezaji wa Ligi ya nchini mwake.
Ngassa aliyesaini Mkataba wa miaka minne na Free State Stars ya Afrika Kusini Mei mwaka huu akitokea Yanga SC ya Tanzania kwa sababu hiyo ameondolewa kikosini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.


Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.
Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.
Continue Reading...

LOWASSA AVUNA ZAIDI YA WADHAMINI 30,000 MKOANI KILIMANJARO.



Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.




 Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780.











Continue Reading...

ACT YAVUNA UMATI MKUBWA KIGOMA.

1

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwapungia mkono wakazi wa mji wa Kigoma jana wakati akiwasili kabla ya kufanya mkutano wahadhara wa kutambulisha viongozi wa chama hicho.

5
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo, Anna Mghwira, akiwapungia mkono wakazi wa mji wa Kigoma jana wakati akiwasili kabla ya kufanya mkutano wahadhara wa kutambulisha viongozi wa chama hicho mkoani kigoma.
6

7
Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akicheza wimbo wa chama ulioimbwa na msanii, Baba Levo, wakati wa mkutano wahadhara mjini Kigoma jana.

2
Baadhi ya wakazi wa mji wa Kigoma wakifuatilia mkutano wa hadhara wa chama cha ACT Wazalendo mjini Kigoma jana.

3

4

Continue Reading...

MAKAMU WARAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA SIKU YA TABIANCHI AFRIKA CHUO KIKUU CHA UDSM



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kuongamano hilo lilifanyika jana Juni 17, 2015 kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa watafiti wa Kituo cha 'Center For Climate Changes Styles', Khalid Mwakobaa (kulia) na Rdith Benedict, wakati alipotembelea katika Mabanda ya maonesho kwenye Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia viatu vya ngozi vinavyotengenezwa na Mtaalamu wa uchakataji wa bidhaa za ngozi, Stephano Chifwaguzi, (kulia) wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonesho katika Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR




Baadhi ya wadau na wanafunzi waliohudhuria Kongamano hilo,wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR
5, 6, 7, 8, 9 na10:- Picha ya pamoja kwa kumbukumbu, baada ya ufunguzi wa Kongamano hilo. Picha na OMR




11:- Makamu wa Rasi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanafunzi  wa Chuo Kikuu UDSM, baada ya kufungua Kongamano la Siku ya Tabianchi Afrika, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya. Kuongamano hilo lilifanyika jana Juni 17, 2015 kwenye Ukumbi wa Nkhurumah Chuo Kikuu Dar es Salaam, jana. Picha na OMR


Continue Reading...

Followers

Follow The Author