Tuesday, November 3, 2015
Tuesday, October 13, 2015
SIKU NANE ZATOLEWA KUHAKIKI TAARIFA KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, akizungumza na wahariri vyombo vya habari Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Jaji Lubuva alisema kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.
“Tume imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura anapata haki ya kupiga kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume katika majukwaa wakati wa kampeni pia amewasaa wanasiasa hao kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.
“Katika kuelekea uchaguzi Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo Tanzania Bara ni vituo 63,525 na Zanzibar ni vituo 1,580 kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema Bw.Ramadhan.
Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.
MO DEWJI KUANZISHA BENKI KUTOA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI.
CEO wa Kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ofisini kwake.
Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji ambaye hivi karibuni amepata tuzo ya Mfanyabiashara Bora wa Afrika wa mwaka 2015, katika kinyang’anyiro cha tuzo za wafanyabiashara bora wa Afrika (African Business Awards 2015) amebainisha kuwa lengo kuu la kampuni anayoiongoza ya MeTL Group, hadi kufikia mwaka 2022, ni kufikia dola bilioni 5 huku akitarajia kuajiri wafanyakazi zaidi ya Laki moja.
Dewji maarufu kama MO amebainisha hayo wakati wa mahojiano maalum ya moja kwa moja yaliyorushwa hivi karibuni na kituo cha BBC kupitia kipindi cha BBC SWAHILI DIRA YA DUNIA ambapo alibainisha hayo.
Kupitia kipindi hicho cha BBC Swahili, MO aliweza kuelezea mafanikio aliyofikia ikiwemo siri ya kufanya kazi kwa bidii na kujituma.
Ambapo ameeleza kuwa, alianza biashara akiwa mdogo sana kwani wakati huo Baba yake alikuwa akimfundisha kazi na yeye kujituma zaidi bila kuchoka.
Aidha, MO amebainisha kuwa, yupo mbioni kuanzisha Benki ya kuweza kutoa mikopo midogo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kujiendeleza.
Salim Kikeke aliweza kumuuliza swali juu ya vijana wengi wanapenda kufanyabiashara lakini hawana mitaji ambapo MO alifunguka kuwa:
“Unajua na mimi mwenyewe nataka kuanzisha ‘Micro credit bank’, ya kuweza kutoa mikopo midogomidogo kwa wafanyabiashara wadogo. Kwa sasa hivi kuna benk nyingi sana zimezidi ukilinganisha mwaka 1998, nilipotoka Marekani, benki zilikuwa ndogo sana kwa hiyo nimeanza kutafuta pesa kutoka benki za Afrika Kusini” ameeleza MO na kuongeza kuwa mtu unapokuwa na wazo la kuanzisha biashara unaweza kushirikiana na mwenye pesa ama kukopa kwa mtu mwenye pesa. alifafanua MO .
Katika mahojiano hayo, MO alibainisha kuwa, mapato katika akaunti ya MeTL GROUP ina kiasi cha dola bilioni 1.3 huku akiwa ameajiri watu zaidi ya 24,000 huku lengo hadi kufikia mwaka 2022, kuwa na wafanyakazi zaidi ya Laki moja huku mapato kuwa zaidi ya dola bilioni 5.
Tuzo aliyopata MO alikabidhiwa katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Four Season mkabala na jengo la Umoja wa Mataifa (Baraza Kuu) watu wengine waliopata tuzo ni Aliko Dangote, Daphne Mashile Nkosi, Strive Masiyiwa na Helen Hai.
MO alimshinda Aliko Dangote ambao walikuwa kwenye Kategori moja wakiwania tuzo hiyo ya mfanyabiashara bora wa Afrika, huku wengine walioshindanishwa kwenye kategori hiyo ni CEO wa Paramount Group, Ivor Ichikowitz, CEO wa Groupe Loukil, Groupe UADH, Bassem Loukil, na Oscar Onyema DG wa Nigerian Stock Exchange.
Sunday, October 11, 2015
JURGEN KLOOP SASA RASMI LIVERPOOL. FERGIE AZUNGUMZIA UTEUZI WAKE...
Jurgen kloop akiwa ameshikilia skafu ya Liverpool Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari.
Klabu ya soka ya Liverpool imemteua Jurgen Klopp kuwa kocha wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.
Klopp, raia wa Ujerumani mwenye miaka 48 anachukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa miaka mitatu na nusu.
Klopp amekuwa nje ya dimba tokea mwezi Mei mwaka huu baada ya kudumu na klabu ya Borussia Dortmund kwa misimu saba.
Anatarajiwa kuanza kazi kwenye klabu hiyo ya Liverpool na wasaidizi wake Zeljko Buvac na Peter Krawietz aliofanya nao kazi akiwa kwenye Ligi ya Bundesliga.
.Kloop Alijiunga Dortmund mwaka 2008 na kuiongoza kushinda vikombe viwili vya ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Klopp, raia wa Ujerumani mwenye miaka 48 anachukua nafasi ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuhudumu katika klabu hiyo kwa miaka mitatu na nusu.
Klopp amekuwa nje ya dimba tokea mwezi Mei mwaka huu baada ya kudumu na klabu ya Borussia Dortmund kwa misimu saba.
Anatarajiwa kuanza kazi kwenye klabu hiyo ya Liverpool na wasaidizi wake Zeljko Buvac na Peter Krawietz aliofanya nao kazi akiwa kwenye Ligi ya Bundesliga.
.Kloop Alijiunga Dortmund mwaka 2008 na kuiongoza kushinda vikombe viwili vya ligi kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
Wakati Kloop akisaini kuifundisha klabu hiyo, aliyekuwa kocha wa zamani wa manchester united Sir Alex Ferguson amezungumzia uteuzi huo.
Sir Ferguson alisema “Ni uteuzi mzuri, namjua vizuri kupitia kwenye mikutano yetu ya darasa la ukocha tukiwa Geneva. Klopp ni mtu makini na pia anapenda kujua kila kitu na kujaribu kukitumia kwenye kazi. Pia anajua nini anakitaka akiwa na mipango yake kama tulivyoona alivyofanya vizuri na Dortmund. Nadhani atafanya vizuri, sitaki kusema hivyo kwasababu ni Liverpool lakini bila shaka lazima atafanya vizuri”
Fergie aliongeza kusema kwamba ni vizuri kama Klopp akifanya kazi mwenyewe bila kuingiliwa na wamiliki, “Kama haumuamini manager wako sasa utamuamini nani? Huyu ndio mtu pekee anatakiwa kusema mchezaji anamtaka na akacheze wapi. Kuna haya mambo ya kibiashara sana kwenye soka, nadhani kuna wakati yanakosewa. Kama haumuamini kocha kwanini umempa kazi. Sidhani kama Klopp atalikubali hili swala”
MWAMBUSI AKARIBIA KUVAA VIATU VYA MKWASA YANGA. MBEYA CITY YABARIKI KUONDOKA KWAKE.
Kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi ameshafikia makubaliano na uongozi wa Yanga ili kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara. Mwambusi anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuchukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa aliyepewa jukumu la kuifundisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Leo mchana Kocha Mkuu wa Mbeya City Fc, Juma Mwambusi, alikutana kwa dharula na mtendaji Mkuu wa klabu (Katibu Mkuu) kwa mazungumzo.
Pamoja na mambo mengine, katika mazungumzo hayo, Mwl Juma Mwambusi alitumia nafasi hiyo kuuaga rasmi uongozi ili kwenda kujiunga na timu ya Young Africans ‘Yanga’ ya Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, katika mazungumzo hayo, Mwl Juma Mwambusi alitumia nafasi hiyo kuuaga rasmi uongozi ili kwenda kujiunga na timu ya Young Africans ‘Yanga’ ya Dar es Salaam.
Katika hali ya kawaida kabisa uongozi wa klabu umekubaliana na kile ambacho Mwl Mwambusi alikisema na kukiomba ikiwa ni kwa ajili ya manufaa ya klabu na manufaa yake kama kocha.
Klabu inachukua fursa hii kumshukuru Mwl. Juma Mwambusi kwa yote mazuri aliyofanya kwenye timu kwa kipindi chote cha miaka mitano ambacho amefanya kazi hapa kwa mafanikio makubwa.
Klabu inachukua fursa hii kumshukuru Mwl. Juma Mwambusi kwa yote mazuri aliyofanya kwenye timu kwa kipindi chote cha miaka mitano ambacho amefanya kazi hapa kwa mafanikio makubwa.
Ikumbukwe kuwa Mwl Juma Mwambusi ni mmoja wa waanzilishi wa timu ya Mbeya City FC, hivyo uongozi unatambua na kuthamini mchango wake mkubwa ndani ya klabu tangu kuanzishwa mpaka hapa ilipofika.
Kwa niaba ya bodi, klabu, inamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya ndani ya klabu ya Young Africans.
Kwa sasa benchi la ufundi la Mbeya City FC litabaki kuwa chini ya kocha msaidizi Meja Abdul Mingange(Rtd.) mpaka itakapotolewa taarifa nyingine.
Kwa sasa benchi la ufundi la Mbeya City FC litabaki kuwa chini ya kocha msaidizi Meja Abdul Mingange(Rtd.) mpaka itakapotolewa taarifa nyingine.
Imetolewa na,
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
KAYUMBA JUMA ANYAKUA MILLIONI 50 ZA BSS. AWABWAGA WENZAKE WATANO
Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.
Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Madam Rita (wa pili kutoka kushoto), akimtangaza mshindi huyo.
Washiriki waliongia kwenye 6 bora ya mashindano hayo wakiwa jukwaani kabla ya mchujo huo kuanz
Mmoja wa Majaji wa shindano hilo (kulia), Master Jay akiingia ukumbini hapo huku akiwa ameongozana na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Bongo fleva Shaa.
Majaji wakiwa kwenye meza yao ya kuratibia mashindano hayo.
Peter Msechu akiwa katika pozi kwenye Red Carpet.
Wasnii wanaounga kundi la Navy Kenzo wakipagawisha jukwaani hapo.
Msanii Kayumba Juma, usiku wa kuamkia jana aliibuka mshindi katika kinyang'anyiro cha kumsaka msanii mwenye kipaji cha kuimba kinachojulikana kama Bongo Star Search baada ya kuwabwaga wenzake watano waliofanikiwa kuingia katika sita bora ya kinyang'anyiro hicho na hivyo kufanikiwa kujinyakulia zawadi ya shilingi millioni 50 kutoka kwa waandaaji wa shindano hilo.
Kayumba aliwabwaga chipukizi wengienwatano ambao ni Frida Amani, Nassibu Fonabo, Jcqueline kayengi, Angel Marry Kato na Kelvin Gerson.
Mashindano hayo yanaandaliwa na kampuni ya Benchmark Production chini ya ukurugenzi wa Ritha Poulsen "Madam Ritha" amabaye ni chief judge wa mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya 8 yakianzia mwaka 2006 ambapo jumanne Idd alifanikiwa kunyakua ubingwa kwa mara ya kwanza.
Mbali na kitita hicho cha million 50, Kayumba pia amefanikiwa kupata bure bima ya afya kwa mwaka mmoja chini ya Jubilee Insurance.
SIKU 13 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, CCM YAFANYA KIKAO CHA DHARULA JANA. DR BILAL ASHIRIKI
wajumbe wa kamati kuu ya CCM wakiwa wamesimama kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki, marehemu Celina Kombani, wakati walipokutana kwa dharula jijini Dar es Salaam, jana Okt 10, 2015. Picha na OMR
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na ........baada ya kumalizika kwa kikao cha dharula, kwenye Ukumbi wa CCM Makao Makuu Lumumba jijini Dar es Salaam,jana Okt 10, 2015. Picha na OMR
Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungabo wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Katibu Mkuu wa CCM, Abrahman Kinana (kushoto) na Mjumbe wa Kamati Kuu, Salim Ahmed Salim (katikati) wakifurahia jambo nje ya ukumbi wa CCM Makao Makuu Lumumba, baada ya kumalizika Kikao cha dharula, jana Okt 10, 2015. Picha na OMR
JOB VACANCY ALERT! NAFASI ZA KAZI TTCL
ONLINE JOB APPLICATIONS
Home Page | |
Job Ref No: | 1341000 |
Job Title: | Logistics Officer Central Ware house |
Post(s): | 1 |
Report To: | Stores Manager |
Closing Date: | Wednesday, October 21, 2015 (16:30) |
Objectives: | |
To ensure qualities of materials management functions are met in order to have qualified practice in the Central ware house in terms of stock and inventory management.
| |
Key Responsibilities: | |
1. To ensure receipt of centrally ordered goods/materials in terms of quantity and quality.
2. To dispatch received goods/materials to the intended users/requisitioner and track the movement to the intended recipients. 3. To ensure there is proper stocks and inventory management/records at the Central Warehouse and alert/advise users on the stock levels of critical materials for appropriate actions. 4. To establish and maintain a smooth interfaces and work relations with the PMU and key stakeholders in the Company. 5. To supervise the stock taking exercise for the Central Ware House and ensure is conducted as scheduled and in an effective manner. 6. To examine and point out shortfalls in the Central Ware House and provide expertise for rectification. 7. Ensures a quality and knit warehouse environments for easy access for a stored goods and materials. 8. To closely work with projects management teams and conduct compliance checks in the company and identifies opportunities for improvement. 9. Provide leadership to the workgroup by mentoring, advising and providing technical expertise. 10. Accountable for allocating tasks to the workgroup and monitoring the work for performance and quality assurance. | |
Key Qualifications / Experience / Skills: | |
• University Degree in Materials Management, Logistics or Business Administration
• At least five (5) years experience in Logistics or a similar field and be recognized as an expert | |
Additional Informations: | |
© 2007 Tanzania Telecommunications Company Limited. All rights reserved.
Friday, August 7, 2015
MKWASA ATANGAZA KIKOSI CHA STARS KUJIANDAA DHIDI YA NIGERIA.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa (pichani juu) leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaoingia kambini siku ya Jumapili tarehe 9, Agosti 2015 katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la Gerezani kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi (Proffesional), ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015 nchini Uturuki.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul - Uturuki, ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).
Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).
Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza)
Thursday, July 30, 2015
MAPYA ZAIDI YAIBUKA CCM. PROF MWANDOSYA ATOA YA MOYONI KUHUSU MCHAKATO WA UTEUZI WA MGOMBEA URAIS CCM.
Mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeendelea kuibua mapya na kuleta mvutano baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya, kunukuliwa akisema kuwa majina matano yaliyopelekwa kwenye Kamati Kuu ya CCM (CC) kutoka kwenye Kamati ya Maadili yalijulikana hata kabla ya kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
PROF MARK MWANDOSYA
Prof. Mwandosya ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki amenukuliwa akisema hayo kwenye sauti yenye maelezo yake iliyorekodiwa na kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Prof. Mwandosya alisema amepata taarifa za kusambazwa kwa sauti hiyo lakini hafahamu kama yanayozungumzwa humo ni ya kwake.
Prof. Mwandosya alisema anachokumbuka akiwa kijijini kwao Lufilio wilayani Rungwe aliitwa na wazee na kufanya nao mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kilichojiri wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais CCM.
“Niliitwa na wazee kwenye mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kimetokea na inawezekana yaliyomo ndani ya hiyo clip yana ukweli, lakini wewe unadhani nilichokisema ni uongo?, Si kinalingana na hali halisi ilivyokuwa Dodoma,” alisema.
Hata hivyo, alisema taarifa zilizosambazwa kwamba anataka kuhamia Chadema siyo za kweli.
Katika sauti iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Prof. Mwandosya amenukuliwa akisema kuwa majina ya makada walioingia tano bora katika kinyang’anyiro cha urais yaliyopelekwa Kamati Kuu yalijulikana hata kabla ya kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
Alisema Mwenyekiti wa Kamati Kuu, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa na majina yake matano mfukoni na kamati yenyewe pia ilikuwa na majina yake.
Akizungumzia madai hayo, Prof. Mwandosya alithibitisha kuwa madai hayo ni ya kweli na kwamba wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM waliokuwapo Dodoma wanalijua hilo.
“Hapo mimi sioni kwamba kuna jambo ambalo limepotoshwa, kwani yote yanayosemwa ni ya kweli na hata wajumbe wote waliokuwa Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wanayajua vizuri mambo hayo,” Prof. Mwandosya.
Alisema ingawa hajaisikia sauti inayodaiwa kuwa ni yake, lakini kama ni suala la kusema kuwa mgombea urais mteule wa CCM, Dk. John Magufuli hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi la CCM ni kweli.
Alizidi kueleza kuwa, anaona ni sahihi kwa sababu katika kumbukumbu zake hajawahi kusikia wala kumwona Dk. Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Chama katika ngazi yoyote.
“Nina kazi nyingi sijafungua mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kidogo, lakini kama mambo yanayosemwa ni hayo, sioni kama kuna uongo ndani yake, ningepata shida sana kama mambo yanayozungumziwa yangekuwa siyo ya kweli, katika kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Dk. Magufuli amekuwa Mwenyekiti wa Chama au Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama, lakini sasa ndiye atakayekuwa mwenyekiti wa Chama chetu nadhani hilo liko wazi,” alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof. Mwandosya alisema kuwa Lowassa ametumia haki yake ya kidemokrasia na yeye haoni kama kwa uamuzi huo amefanya kosa lolote.
Alisema vyama vya siasa ni sawa na madhehebu ya dini, ambapo waumini wanayo haki ya kwenda kuabudu katika kanisa wanalolitaka au ambalo imani yao inawatuma na hakuna mtu wa kuwapokonya haki hiyo.
“Alichokiamua Lowassa sidhani kama ana kosa, kwani anayo haki na uhuru wa kufanya alichokifanya, siku hizi kuna makanisa mengi, mtu anapoamua kwenda kuabudu katika kanisa analoona linamfaa huwezi kusema kuwa amekosea, labda ninachoweza kushauri ni CCM kujiuliza sababu za Lowassa kuondoka na ikiwezekana ijisahihishe ili watu wengi zaidi wasiondoke,” alisema.
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE NCHINI AUSTRALIA.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa
Labels:
MATUKIO
MH LOWASSA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA MAPEMA LEO. ANGALIA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA,
Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema. Hatua hiyo inafuatia matukio ya jina lake kukatwa na kutokupitishwa na chama tawala ambapo mh lowassa aliomba kuteuliwa na kukosa nafasi hiyo,
Mapema mwanzoni mwa wiki hii Mh lowassa alitambulishwa rasmi kujiunga na chadema na hivyo kupewa tena nafasi ya kugombea uraisi wa JMT kupitia chadema na baadae UKAWA ambao ni muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho, 
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,
Mwenyekiti wa chadema, mh freeman mbowe akiteta jambo na Mh lowassa wakati wa hafla ya Mh lowassa kukabidhiwa rasmi fomu ya kugombea urais ya chadema mapema leo.
Mwenyekiti wa chadema mh Freeman Mbowe akimkabidhi mh Lowassa fomu ya kugombea urais kupitia chadema, mapema leo jijini Dar Es Salaam.
Mh Lowassa akiteta jambo na Mwanasheria mkuu wa chadema na mbunge wa singida mh Tundu lissu mapema leo wakati mh Lowassa akichukua fomu ya kugombea urais kupitia chadema.
akizungumza wakati wa dhima hiyo mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho hivyo kufuta uvumi uliokuwa ukienea kuwa yeye (lissu) pamoja na katibu mkuu wilbroad slaa wamesusa na hawajapendezwa na tukio la lowassa kukaribishwa chadema.
Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.
Labels:
MATUKIO
RAIA WAKIGENI 2040 WAKAMATWA WAKIWA NA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA
Raia wa kigeni wajaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wafikia 2040 kwa mikoa ya mikoa ya Kagera watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65.
Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Dar es Salaam leo.
Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa.
Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.
Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale.
Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa.
Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.
Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale.
Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na wahamiaji haramu wanayo jiandikisha katika Daftari la wapiga kura katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa uhamiaji wilaya ya Iala, Safina Muhindi,katikati ni Afisa uhamiaji wilaya ya Temeke, Jaffari Kisesa na Afisa Mdhibiti wa Paspoti, Cripin Ngonyani wakimsikiliza Kaimu kamishina wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Da es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo
Labels:
MATUKIO
Friday, July 24, 2015
BVR DAR YASUASUA. WANANCHI WATWANGANA
Wakati uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ukiingia siku ya tatu leo, kasoro lukuki zimeendelea kugubika mchakato huo huku katika baadhi ya vituo wananchi wakizichapa wakigombania kuingia chumba cha kujiandikisha.
Tukio la kutwangana makonde lilitokea katika Kituo cha Shule ya Mwangaza, Gongo la Mboto saa 2.15 asubuhi wakati uandikishaji ulipokuwa ukianza.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema: “Polisi unaowaona wamefika muda si mrefu, wala hawakuwepo hapa tangu asubuhi... ninadhani walipewa taarifa baada ya watu kuanza fujo wakigombania kuingia ndani kujiandikisha,” alisema Magreth John na kuongeza:
“Watu wamepigana kwa sababu wanasema kuna wenzao ambao majina yao hayakuandikwa jana (juzi) halafu wamefika asubuhi wakaanza kuitwa ndani kujiandikisha. Hapo ndipo mzozo ulipoanzisha na ngumi zikafumuka.”
Msimamizi wa kituo hicho, Ramadhani Mshindo alisema mzozo huo ulitokea kwa sababu ya wananchi hao hawakuelewa utaratibu.
“Jana (juzi) jioni wakati tunafunga zoezi hili saa 12.00 jioni kuna watu wengi walikuwa kwenye foleni ambao hawakuandikishwa, kwa hiyo tuliwaandika majina ili leo (jana) wakifika hapa watangulie kuandikishwa kabla ya wengine. Sasa tulivyofika na kuanza kuita majina yao ili waingie kujiandikisha ndipo watu wakaanza fujo na kupigana ikabidi tupige simu polisi ili waje kutuliza ghasia,” alisema Mshindo.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Jica, Tabata wananchi walilalamikia suala la muda kwani waandikishaji walichelewa na hadi saa 4.30 asubuhi, asilimia kubwa ya watu hawakuwa wamepata huduma. “Nimefika hapa saa 12.00 asubuhi lakini hadi sasa sioni dalili ya kuandikishwa leo… Wametuambia wanaanza kuandikisha wale waliobaki jana kwa sababu majina yao yaliandikwa kwa hiyo sisi wa leo tunasubiri kwanza,” alisema Maria Saleh.
Maria alisema uandikishaji unakwenda taratibu kutoka na mashine kugoma mara kwa mara.
Malalamiko kama hayo yalitolewa na wananchi waliokuwa wamefika kujiandikisha katika Kituo cha Shule ya Msingi, Ulongoni, Gongo la Mboto na waandishi wetu walishuhudia watu wengi wakiwa kwenye misururu, wengine wakiwa wamelala pembeni ya kituo hicho baada ya kuchoka kusimama muda mrefu.
Hata hivyo, kwenye kituo hicho, wananchi walijiwekea utaratibu kwamba kila mtu anayefika anaandika namba kwenye daftari na kupewa kikaratasi kidogo chenye namba hiyo ndipo anapanga foleni.
Utaratibu ambao ulisaidia kupunguza usumbufu na kuondoa vuta ni kuvute wakati wa kuingia kwenye chumba cha kujiandikisha.
Lakini licha ya kujiweka utaratibu huo, Ibrahim Kitumbi alisema changamoto ya muda na vifaa ilikuwa palepale.
“Hivi tunavyozungumza watu waliyopewa namba wamefika 2,145. Hawa wameandika majina tu na kupewa namba. Waliojiandikisha tangu jana hawafiki hata 200. Sasa kwa siku nane zilizobaki kweli tunaweza kumaliza kuandikishwa! Huku si kutunyima haki?” alihoji.
Wakati wananchi wakitoa malalamiko hayo, Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Ulongoni, Majura Mtalemwa alisema zoezi la uandikishaji linakwenda vizuri tofauti na wananchi wanavyolilalamikia.
Mkazi wa Temeke, Steven Almasi aliyefika kujiandikisha katika Kituo cha Magogoni, Yombo alisema mwaka huu wa uchaguzi kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya wananchi kutoshiriki uchaguzi.
Mtendaji wa mtaa huo, Zeddy Zeddy alikiri kuwapo baadhi changamoto kwenye kituo chake ikiwamo uchache wa mashine za kuandikisha.
“Mwitiko wa watu umekuwa mkubwa tofauti na matarajio yetu kwa hiyo kama mashine zikiongezwa kwenye baadhi ya vituo, itasaidia kuondoa msongamano na kazi kukamilika kwa wakati,” alisema Zeddy.
“Kama Tume ingeongeza mashine, mambo yangekwenda vizuri zaidi lakini kinachoendelea ni ngumu kusema kuwa watu wote wataandikishwa kama ilivyopangwa,” alisema mtaalamu wa BVR aliyekuwapo Kituo cha Shule ya Msingi Kibangu, Ubungo, Suleiman Mahmoud.
Katika kituo cha Kontena – Tanesco, Kinondoni ni mashine moja tu iliyokuwa ikifanya kazi kati ya tatu kutokana na kuharibika licha ya idadi ya watu kuwa wachache.
“Mashine moja ilikuwa haifanyi kazi hadi saa tatu asubuhi, wameleta nyingine lakini nayo kamera inasumbua. Hii yangu printa haifanyi kazi hivyo ipo moja tu. Tumewapigia IT (mafundi wa Teknolojia ya Mawasiliano) wamesema wanakuja lakini wengi wanatembea kwa miguu wanachelewa kufika,” alisema mwendeshaji mashine ya BVR kituoni hapo, Max Phillipo.
Mkazi wa Mwananyamala, Hemed Shefaya alisema alifika kituoni tangu saa 10 alfajiri akiwa na wenzake watatu lakini kilifunguliwa saa 2.30 asubuhi.
“Mashine hizi zinaharibika mara kwa mara, kwa sasa wamezitengeneza lakini mikono ya wasimamizi ni mizito sana. Tulikuja jana na kupatiwa namba lakini hatukufanikiwa kuandikishwa… fikiria mimi namba 18 ya jana nimekuja saa 12 asubuhi lakini bado hadi sasa (saa 5.43) sijaandikishwa,” alisema Ramadhani Mkombozi aliyekuwa katika Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani, Mwananyamala.
Ofisa Uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni, Valence Urassa alisema tatizo la kuharibika kwa BVR lilikuwa likifanyiwa kazi na mafundi wa NEC na Manispaa na kwamba maeneo yenye wakazi wengi yalikuwa yakiongezwa mashine kufikia mbili kila kituo.
Kuhusu kuchelewesha kufungua vituo, alisema kituo chochote hakitafunguliwa 2.00 asubuhi iwapo waandikishaji hawatakuwa wamekamilisha maandalizi ya vifaa na kuandikisha kwani kuwahisha kutaleta matatizo.
Baadhi ya wasimamizi wametoa wito kwa NEC kuongeza vifaa pamoja na wataalamu ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.
Msimamizi wa Kituo cha Chuo cha Usafirishaji (NIT), Kelvin Donald alisema mashine alizonazo zinasumbua tangu juzi na hata baada ya kutoa taarifa na kubadilishiwa bado tatizo hilo linaendelea.
“Kwa wastani wanajitokeza watu 1,200 kila siku na hapa tuna mashine tano tu, moja haifanyi kazi,” alisema Donald.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Luis, Omari Mshauri alisema baada ya umeme kuwa kikwazo, juzi msamaria mmoja alijitolea jenereta huku wengine wakichangia mafuta kuendelea na kazi.
NEC yafafanua
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Malaba alisema wakazi wote wa jiji hili waliojitokeza wataandikishwa hata baada ya siku zilizopangwa kumalizika hivyo hawatakiwi kuwa na hofu.
“Hakuna mtu aliyejitokeza kuandikishwa halafu akaachwa… tutaandikisha mpaka wote waliojitokeza siku ya mwisho watakapokamilika.
“Mpaka sasa tuna mashine takriban 3,500 na nyingine zinaendelea kuingia kutoka mikoa ambayo tumeshakamilisha kuandikisha. Hizi zote zitaletwa kuongeza nguvu ya uandikishaji katika maeneo yenye wakazi wengi na kumaliza haraka,” alisema Malaba.
Kawe kujiandikisha upya
Malaba alieleza kuwa wakazi wa Jimbo la Kawe ambao walijiandikisha awali katika uandikishaji wa majaribio, watatakiwa kujiandikisha upya ili wapate vitambulisho vya sasa.
Hata hivyo, hakutaja sababu za kurudia na kuahidi kufafanua zaidi leo.
RC atoa maagizo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amewataka wakurugenzi wote wa Manispaa za Dar es Salaam kutoka maofisini na kwenda kusimamia kwa karibu uandikishaji huo na kutatua matatizo yanayoripotiwa na wananchi kila wakati.
Alisema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, mojawapo likiwa waandikishaji kuchelewa kufika vituoni, kuwahi kuondoka kabla ya muda na mashine kugoma.
“Tutachukua hatua kali kwa ofisa mwandikishaji yeyote atakayekiuka taratibu na kukwamisha uandikishaji... tunafahamu uandikishaji unakabiliwa na changamoto nyingi, lakini nimepata taarifa kuwa waandikishaji pia wanahujumu uandikishaji bila sababu za msingi,” alisema Sadik
Subscribe to:
Posts (Atom)
Followers
Follow The Author
Designed By Templateism | Seo Blogger Templates