Thursday, July 30, 2015

MH LOWASSA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA MAPEMA LEO. ANGALIA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA,

Share it Please
Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema. Hatua hiyo inafuatia matukio ya jina lake kukatwa na kutokupitishwa na chama tawala ambapo mh lowassa aliomba kuteuliwa na kukosa nafasi hiyo,
Mapema mwanzoni mwa wiki hii Mh lowassa alitambulishwa rasmi kujiunga na chadema na hivyo kupewa tena nafasi ya kugombea uraisi wa JMT kupitia chadema na baadae UKAWA ambao ni muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho, 
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,

Mwenyekiti wa chadema, mh freeman mbowe akiteta jambo na Mh lowassa wakati wa hafla ya Mh lowassa kukabidhiwa rasmi fomu ya kugombea urais ya chadema mapema leo.
Mwenyekiti wa chadema mh Freeman Mbowe akimkabidhi mh Lowassa fomu ya kugombea urais kupitia chadema, mapema leo jijini Dar Es Salaam.
Mh Lowassa akiteta jambo na Mwanasheria mkuu wa chadema na mbunge wa singida mh Tundu lissu mapema leo wakati mh Lowassa akichukua fomu ya kugombea urais kupitia chadema.



akizungumza  wakati wa dhima hiyo mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho hivyo kufuta uvumi uliokuwa ukienea kuwa yeye (lissu) pamoja na katibu mkuu wilbroad slaa wamesusa na hawajapendezwa na tukio la lowassa kukaribishwa chadema.
Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.
Mh Lowassa akizungumza na mh Mchungaji Msigwa,

Mh Godbless Lema pia alikuwa ni mmoja ya waliohudhuria dhifa hiyo ya mh Lowass kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chadema, mapema leo.

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author