Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva, akizungumza na wahariri vyombo vya habari Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Julius Mallaba.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wapiga kura kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya kupiga kura siku nane kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva alipokuwa akizungumza katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika jijini Dar es Salaam,
Jaji Lubuva alisema kuwa lengo la mkutano huo lilikuwa ni kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.
“Tume imepanga kuhakikisha kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura anapata haki ya kupiga kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume katika majukwaa wakati wa kampeni pia amewasaa wanasiasa hao kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya daftari la kudumu la kupiga kura.
“Katika kuelekea uchaguzi Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo Tanzania Bara ni vituo 63,525 na Zanzibar ni vituo 1,580 kila kituo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500 kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema Bw.Ramadhan.
Mpaka sasa tume imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi karibuni.