Saturday, July 4, 2015

KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER YAFANYIKA DAR.

Share it Please

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick akizindua kampeni ya kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani ( MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Nd.Assah Mwambene akikabidhi kiasi cha fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa kampeni ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bw.Benjamin Thomson,zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa Habari wa Serikali ,walijitolea kuchanga kiasi cha shilingi 1,680,000=.
Pichani kati anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda

Kama vile haitoshi nayo Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia walifanikisha kuchangia kiasi cha shilingi 1,350,000/= kufuatia kuguswa kwa namna moja nyingine kwa kampeni  hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani.

Mbali ya fedha hizo kupatikana pia walijitokeza watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER,ambalo kwa kiasi kikubwa bado linahitaji kuongeza hamasa zaidi ili wadau wazidi kujitokeza na kuchangia.

Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha,huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mh said Meck  Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika MEDIA CAR WASH FOR CANCER. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Issa Michuzi wa Libeneke la Michuzi Blog na Michuzi Media Group akitimiza majukumu... Anaosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangia waandishi wa habari ambao wana maradhi ya Saratani mapema leo kwenye kampeni.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Assah Mwambene akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi zima la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Picha ya pamoja ya waandishi wa Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi 

No comments:

Post a Comment

Followers

Follow The Author