Thursday, July 30, 2015

MAPYA ZAIDI YAIBUKA CCM. PROF MWANDOSYA ATOA YA MOYONI KUHUSU MCHAKATO WA UTEUZI WA MGOMBEA URAIS CCM.

Mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeendelea kuibua mapya na kuleta mvutano baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya, kunukuliwa akisema kuwa majina matano yaliyopelekwa kwenye Kamati Kuu ya CCM (CC) kutoka kwenye Kamati ya Maadili yalijulikana hata kabla ya kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
PROF MARK MWANDOSYA
Prof. Mwandosya ambaye ni Mbunge wa Rungwe Mashariki amenukuliwa akisema hayo kwenye sauti yenye maelezo yake iliyorekodiwa na kusambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Prof. Mwandosya alisema amepata taarifa za kusambazwa kwa sauti hiyo lakini hafahamu kama yanayozungumzwa humo ni ya kwake.
Prof. Mwandosya alisema anachokumbuka akiwa kijijini kwao Lufilio wilayani Rungwe aliitwa na wazee na kufanya nao mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kilichojiri wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais CCM.
“Niliitwa na wazee kwenye mkutano wa ndani wakitaka kujua nini kimetokea na inawezekana yaliyomo ndani ya hiyo clip yana ukweli, lakini wewe unadhani nilichokisema ni uongo?, Si kinalingana na hali halisi ilivyokuwa Dodoma,” alisema.
Hata hivyo, alisema taarifa zilizosambazwa kwamba anataka kuhamia Chadema siyo za kweli.
Katika sauti iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Prof. Mwandosya amenukuliwa akisema kuwa majina ya makada walioingia tano bora katika kinyang’anyiro cha urais yaliyopelekwa Kamati Kuu yalijulikana hata kabla ya kikao cha Kamati ya Maadili hakijaketi.
Alisema Mwenyekiti wa Kamati Kuu, Rais Jakaya Kikwete, alikuwa na majina yake matano mfukoni na kamati yenyewe pia ilikuwa na majina yake.
Akizungumzia madai hayo, Prof. Mwandosya alithibitisha kuwa madai hayo ni ya kweli na kwamba wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM waliokuwapo Dodoma wanalijua hilo.
“Hapo mimi sioni kwamba kuna jambo ambalo limepotoshwa, kwani yote yanayosemwa ni ya kweli na hata wajumbe wote waliokuwa Dodoma kwenye Mkutano Mkuu wanayajua vizuri mambo hayo,” Prof. Mwandosya.
Alisema ingawa hajaisikia sauti inayodaiwa kuwa ni yake, lakini  kama ni suala la kusema kuwa mgombea urais mteule wa CCM, Dk. John Magufuli hajawahi kuwa hata mwenyekiti wa tawi la CCM ni kweli.
Alizidi kueleza kuwa, anaona ni sahihi kwa sababu katika kumbukumbu zake hajawahi kusikia wala kumwona Dk. Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Chama katika ngazi yoyote.
Nina kazi nyingi sijafungua mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kidogo, lakini kama mambo yanayosemwa ni hayo, sioni kama kuna uongo ndani yake, ningepata shida sana kama mambo yanayozungumziwa yangekuwa siyo ya kweli, katika kumbukumbu zangu sijawahi kusikia Dk. Magufuli amekuwa Mwenyekiti wa Chama au Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama, lakini sasa ndiye atakayekuwa mwenyekiti wa Chama chetu nadhani hilo liko wazi,” alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof. Mwandosya alisema kuwa Lowassa ametumia haki yake ya kidemokrasia na yeye haoni kama kwa uamuzi huo amefanya kosa lolote.
Alisema vyama vya siasa ni sawa na madhehebu ya dini, ambapo waumini wanayo haki ya kwenda kuabudu katika kanisa wanalolitaka au ambalo imani yao inawatuma na hakuna mtu wa kuwapokonya haki hiyo.
“Alichokiamua Lowassa sidhani kama ana kosa, kwani anayo haki na uhuru wa kufanya alichokifanya, siku hizi kuna makanisa mengi, mtu anapoamua kwenda kuabudu katika kanisa analoona linamfaa huwezi kusema kuwa amekosea, labda ninachoweza kushauri ni CCM kujiuliza sababu za Lowassa kuondoka na ikiwezekana ijisahihishe ili watu wengi zaidi wasiondoke,” alisema.
Continue Reading...

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA NEWCASTLE NCHINI AUSTRALIA.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
  Sehemu ya Watanzania waishio nchini Australia wakipiga makofi wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Mama Salma Kikwete akimpongeza mume wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Newcastle na mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ujumbe alioongozana nao mkewe Mama Salma kikwete na mwana wao Ali Kikwete baada ya kutunukiwa shahada.
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja mkewe Mama Salma kikwete, mwana wao Ali Kikwete na Watanzania waishio Australia baada ya kutunukiwa
Continue Reading...

MH LOWASSA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS KUPITIA CHADEMA MAPEMA LEO. ANGALIA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA,

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa amechukua Fomu rasmi ya kugombea urais kupitia tiketi ya Chadema. Hatua hiyo inafuatia matukio ya jina lake kukatwa na kutokupitishwa na chama tawala ambapo mh lowassa aliomba kuteuliwa na kukosa nafasi hiyo,
Mapema mwanzoni mwa wiki hii Mh lowassa alitambulishwa rasmi kujiunga na chadema na hivyo kupewa tena nafasi ya kugombea uraisi wa JMT kupitia chadema na baadae UKAWA ambao ni muunganiko wa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa akiwa sambamba na Mkewe Mama Reginal akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar hivi punde ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho, 
Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Edward Lowassa pichani akiwapungia wanachama na wafuasi mbalimbali wa chama cha CHADEMA waliofika kumshuhudia akiwa sambamba na Mkewe Mama Regina akiwasili makao Makuu ya chama cha CHADEMA yaliyopo Kinondoni jijini Dar ,kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais kupitia chama hicho,

Mwenyekiti wa chadema, mh freeman mbowe akiteta jambo na Mh lowassa wakati wa hafla ya Mh lowassa kukabidhiwa rasmi fomu ya kugombea urais ya chadema mapema leo.
Mwenyekiti wa chadema mh Freeman Mbowe akimkabidhi mh Lowassa fomu ya kugombea urais kupitia chadema, mapema leo jijini Dar Es Salaam.
Mh Lowassa akiteta jambo na Mwanasheria mkuu wa chadema na mbunge wa singida mh Tundu lissu mapema leo wakati mh Lowassa akichukua fomu ya kugombea urais kupitia chadema.



akizungumza  wakati wa dhima hiyo mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu amesema baada ya kuchukua fomu hizo Lowassa atakuwa tayari kuzunguka nchi nzima kujitambulisha kwa wananchi kama mgombea rasmi wa Chadema.
Lissu amesema uamuzi wa kumsimamisha mgombea huyo haukuwa wa kukurupuka bali umefuata uchunguzi wa muda usiopungua miezi mitatu na kujiridhisha kuwa Lowassa anafaa kuwa mgombea urais chini ya chama hicho hivyo kufuta uvumi uliokuwa ukienea kuwa yeye (lissu) pamoja na katibu mkuu wilbroad slaa wamesusa na hawajapendezwa na tukio la lowassa kukaribishwa chadema.
Amesema katiba ya Tanzania inasema pamoja na mambo mengine mtu pakee anayezuiwa kugombea urais ni yule aliyekutwa na hatia na Mahakama ndani ya kipindi cha miaka mitano, hivyo Chadema imepekua Nyaraka zote za kimahakama nchini na kujiridhisha kwamba Lowassa hana hatia yoyote inayoweza kumzuia kugombea nafasi ya urais.
Mh Lowassa akizungumza na mh Mchungaji Msigwa,

Mh Godbless Lema pia alikuwa ni mmoja ya waliohudhuria dhifa hiyo ya mh Lowass kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia chadema, mapema leo.
Continue Reading...

RAIA WAKIGENI 2040 WAKAMATWA WAKIWA NA VITAMBULISHO VYA KUPIGIA KURA

Raia wa kigeni wajaribu kujipatia vitambulisho vya kupigia kura wafikia 2040 kwa mikoa ya  mikoa ya Kagera watu 708, Mara 619, Tanga 348,Kigoma 254, Rukwa 13, Kilimanjaro 12, Ruvuma 9, Geita 6, Shinyanga 7, Mtwara 3, Pwani 2, Mbeya 1, Morogoro 1 na Dar es Salaam 65. 
Hayo yamesemwa na Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao  jijini Dar es Salaam leo.

 Aidha Irovya amesema amewakumbusha wananchi kupiga kura ni haki ya kila mwananchi wa Tanzania ana sio raia wa kigeni kujiandikisha ili apige kura kwana raia wa kigeni hana uwezo wa kupiga kura katika nchi asiko zaliwa. 

Pia Irovya amesema kuwa wananchi walio chukua paspoti za kusafiria zinapoisha muda wake ni lazima wabadilishe na kupewa nyingine wakati wowote wanapohitaji.
  
 Irovya ameongezea kuwa wananchi wanaotafuta paspoti za kusafiria tofauti na ofisi za uhamiaji wajue huko wanapotea paspoti zote zinapatikana katika ofisi za uhamiaji tuu na sio popote pale.
 
Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na wahamiaji haramu wanayo jiandikisha katika  Daftari la wapiga kura katika mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kutoka kushoto ni Naibu Kamishna wa uhamiaji wilaya ya Iala, Safina Muhindi,katikati ni Afisa  uhamiaji wilaya ya Temeke, Jaffari Kisesa na Afisa Mdhibiti wa Paspoti, Cripin Ngonyani wakimsikiliza Kaimu kamishina wa uhamiaji Abasi Irovya wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano ofisini kwao jijini Da es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu kamishna wa uhamiaji Abasi Irovya jijin Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo
Continue Reading...

Friday, July 24, 2015

BVR DAR YASUASUA. WANANCHI WATWANGANA

Wakati uandikishaji wa wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, ukiingia siku ya tatu leo, kasoro lukuki zimeendelea kugubika mchakato huo huku katika baadhi ya vituo wananchi wakizichapa wakigombania kuingia chumba cha kujiandikisha.
Tukio la kutwangana makonde lilitokea katika Kituo cha Shule ya Mwangaza, Gongo la Mboto saa 2.15 asubuhi wakati uandikishaji ulipokuwa ukianza.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema: “Polisi unaowaona wamefika muda si mrefu, wala hawakuwepo hapa tangu asubuhi... ninadhani walipewa taarifa baada ya watu kuanza fujo wakigombania kuingia ndani  kujiandikisha,” alisema Magreth John na kuongeza:
“Watu wamepigana kwa sababu wanasema kuna wenzao ambao majina yao hayakuandikwa jana (juzi) halafu wamefika asubuhi wakaanza kuitwa ndani kujiandikisha. Hapo ndipo mzozo ulipoanzisha na ngumi zikafumuka.”
Msimamizi wa kituo hicho, Ramadhani Mshindo alisema mzozo huo ulitokea kwa sababu ya wananchi hao hawakuelewa utaratibu.
“Jana (juzi) jioni wakati tunafunga zoezi hili saa 12.00 jioni kuna watu wengi walikuwa kwenye foleni ambao hawakuandikishwa, kwa hiyo tuliwaandika majina ili leo (jana) wakifika hapa watangulie kuandikishwa kabla ya wengine. Sasa tulivyofika na kuanza kuita majina yao ili waingie kujiandikisha ndipo watu wakaanza fujo na kupigana ikabidi tupige simu polisi ili waje kutuliza ghasia,” alisema Mshindo.
Katika Kituo cha Shule ya Msingi Jica, Tabata wananchi walilalamikia suala la muda kwani waandikishaji walichelewa na hadi saa 4.30 asubuhi, asilimia kubwa ya watu hawakuwa wamepata huduma. “Nimefika hapa saa 12.00 asubuhi lakini hadi sasa sioni dalili ya kuandikishwa leo… Wametuambia wanaanza kuandikisha wale waliobaki jana kwa sababu majina yao yaliandikwa kwa hiyo sisi wa leo tunasubiri kwanza,” alisema Maria Saleh.
Maria alisema uandikishaji unakwenda taratibu kutoka na mashine kugoma mara kwa mara.
Malalamiko kama hayo yalitolewa na wananchi waliokuwa wamefika kujiandikisha katika Kituo cha Shule ya Msingi, Ulongoni, Gongo la Mboto na waandishi wetu walishuhudia watu wengi wakiwa kwenye misururu, wengine wakiwa wamelala pembeni ya kituo hicho baada ya kuchoka kusimama muda mrefu.
Hata hivyo, kwenye kituo hicho, wananchi walijiwekea utaratibu kwamba kila mtu anayefika anaandika namba kwenye daftari na kupewa kikaratasi kidogo chenye namba hiyo ndipo anapanga foleni.
Utaratibu ambao ulisaidia kupunguza usumbufu na kuondoa vuta ni kuvute wakati wa kuingia kwenye chumba cha kujiandikisha.
Lakini licha ya kujiweka utaratibu huo, Ibrahim Kitumbi alisema changamoto ya muda na vifaa ilikuwa palepale.
“Hivi tunavyozungumza watu waliyopewa namba wamefika 2,145. Hawa wameandika majina tu na kupewa namba. Waliojiandikisha tangu jana hawafiki hata 200. Sasa kwa siku nane zilizobaki kweli tunaweza kumaliza kuandikishwa! Huku si kutunyima haki?” alihoji.
Wakati wananchi wakitoa malalamiko hayo, Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Ulongoni, Majura Mtalemwa alisema zoezi la uandikishaji linakwenda vizuri tofauti na wananchi wanavyolilalamikia.
Mkazi wa Temeke, Steven Almasi aliyefika kujiandikisha katika Kituo cha Magogoni, Yombo  alisema mwaka huu wa uchaguzi kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya wananchi kutoshiriki uchaguzi.
Mtendaji wa mtaa huo, Zeddy Zeddy alikiri kuwapo baadhi changamoto kwenye kituo chake ikiwamo uchache wa mashine za kuandikisha.
“Mwitiko wa watu umekuwa mkubwa tofauti na matarajio yetu kwa hiyo kama mashine zikiongezwa kwenye baadhi ya vituo, itasaidia kuondoa msongamano na kazi kukamilika kwa wakati,” alisema Zeddy.
“Kama Tume ingeongeza mashine, mambo yangekwenda vizuri zaidi lakini kinachoendelea ni ngumu kusema kuwa watu wote wataandikishwa kama ilivyopangwa,” alisema mtaalamu wa BVR aliyekuwapo Kituo cha Shule ya Msingi Kibangu, Ubungo, Suleiman Mahmoud.
Katika kituo cha Kontena – Tanesco, Kinondoni ni mashine moja tu iliyokuwa ikifanya kazi kati ya tatu kutokana na kuharibika licha ya idadi ya watu kuwa wachache.
“Mashine moja ilikuwa haifanyi kazi hadi saa tatu asubuhi, wameleta nyingine lakini nayo kamera inasumbua. Hii yangu printa haifanyi kazi hivyo ipo moja tu. Tumewapigia IT (mafundi wa Teknolojia ya Mawasiliano) wamesema wanakuja lakini wengi wanatembea kwa miguu wanachelewa kufika,” alisema mwendeshaji mashine ya BVR kituoni hapo, Max Phillipo.
Mkazi wa Mwananyamala, Hemed Shefaya alisema alifika kituoni tangu saa 10 alfajiri akiwa na wenzake watatu lakini kilifunguliwa saa 2.30 asubuhi.
“Mashine hizi zinaharibika mara kwa mara, kwa sasa wamezitengeneza lakini mikono ya wasimamizi ni mizito sana. Tulikuja jana na kupatiwa namba lakini hatukufanikiwa kuandikishwa… fikiria mimi namba 18 ya jana nimekuja saa 12 asubuhi lakini bado hadi sasa (saa 5.43) sijaandikishwa,” alisema Ramadhani Mkombozi aliyekuwa katika Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani, Mwananyamala.
Ofisa Uchaguzi wa Manispaa ya Kinondoni, Valence Urassa alisema tatizo la kuharibika kwa BVR lilikuwa likifanyiwa kazi na mafundi wa NEC na Manispaa na kwamba maeneo yenye wakazi wengi yalikuwa yakiongezwa mashine kufikia mbili kila kituo.
Kuhusu kuchelewesha kufungua vituo, alisema kituo chochote hakitafunguliwa 2.00 asubuhi iwapo waandikishaji hawatakuwa wamekamilisha maandalizi ya vifaa na kuandikisha kwani kuwahisha kutaleta matatizo.
Baadhi ya wasimamizi wametoa wito kwa NEC kuongeza vifaa pamoja na wataalamu ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.
Msimamizi wa Kituo cha Chuo cha Usafirishaji (NIT), Kelvin Donald alisema mashine alizonazo zinasumbua tangu juzi na hata baada ya kutoa taarifa na kubadilishiwa bado tatizo hilo linaendelea.
“Kwa wastani wanajitokeza watu 1,200 kila siku na hapa tuna mashine tano tu, moja haifanyi kazi,” alisema Donald.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Luis, Omari Mshauri alisema baada ya umeme kuwa kikwazo, juzi msamaria mmoja alijitolea jenereta huku wengine wakichangia mafuta kuendelea na kazi.
NEC yafafanua
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Malaba alisema wakazi wote wa jiji hili waliojitokeza wataandikishwa hata baada ya siku zilizopangwa kumalizika hivyo hawatakiwi kuwa na hofu.
“Hakuna mtu aliyejitokeza kuandikishwa halafu akaachwa… tutaandikisha mpaka wote waliojitokeza siku ya mwisho watakapokamilika.
“Mpaka sasa tuna mashine takriban 3,500 na nyingine zinaendelea kuingia kutoka mikoa ambayo tumeshakamilisha kuandikisha. Hizi zote zitaletwa kuongeza nguvu ya uandikishaji katika maeneo yenye wakazi wengi na kumaliza haraka,” alisema Malaba.
Kawe kujiandikisha upya
Malaba alieleza kuwa wakazi wa Jimbo la Kawe ambao walijiandikisha awali katika uandikishaji wa majaribio, watatakiwa kujiandikisha upya ili wapate vitambulisho vya sasa.
Hata hivyo, hakutaja sababu za kurudia na kuahidi kufafanua zaidi leo.
RC atoa maagizo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amewataka wakurugenzi wote wa Manispaa za Dar es Salaam kutoka maofisini na kwenda kusimamia kwa karibu uandikishaji huo na kutatua matatizo yanayoripotiwa na wananchi kila wakati.
Alisema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, mojawapo likiwa waandikishaji kuchelewa kufika vituoni, kuwahi kuondoka kabla ya muda na mashine kugoma.
“Tutachukua hatua kali kwa ofisa mwandikishaji yeyote atakayekiuka taratibu na kukwamisha uandikishaji... tunafahamu uandikishaji unakabiliwa na changamoto nyingi, lakini nimepata taarifa kuwa waandikishaji pia wanahujumu uandikishaji bila sababu za msingi,” alisema Sadik
Continue Reading...

Sunday, July 5, 2015

ILANI YA UCHAGUZI CCM YAIVA.

Kamati kuu ya CCM ikiongozwa na mh. dk. Jakaya Kikwete ikiwa kwenye mkutano wa kupitisha ilani ya chama katika ukumbi wa white house ,Dodoma.
KIKAO Maalumu cha Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza jana Mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Kikao hicho ni mwanzo wa vikao vinavyotarajiwa kuanza mapema wiki ijayo, kwa ajili ya kuchuja majina ya walioomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya muda wa kurejesha fomu kwa wanaowania kuteuliwa kugombea urais kumalizika, vikao mbalimbali vya uchujaji wa majina ya wagombea vinatarajiwa kuanza vikitanguliwa na Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili kitakachokutana Julai 8, mwaka huu.
Kikao cha Kamati Kuu kinachotakiwa kujadili wagombea 38 na kuja na majina yasiyozidi matano kinatarajiwa kukutana Julai 9.
Majina hayo yasiyozidi matano, yanatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, ambayo itakutana Julai 10.
Kikao hicho cha NEC, kinatarajiwa kupitia majina hayo na kuja na majina matatu, yatakayopelekwa katika Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 11 na Julai 12 utakaoteua jina moja la mgombea urais wa CCM, baada ya kupigiwa kura na wajumbe wote wa mkutano huo.
CC maalumu Zanzibar
Wakati huo huo, Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya (CCM) Zanzibar, inatarajiwa kukutana kesho mjini Zanzibar kupendekeza jina la mgombea wa urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo la Makao Makuu ya CCM, White House Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Vuai Ally Vuai, alisema kikao hicho maalumu kitafanyika katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya chama hicho Kisiwandui Zanzibar.
Alisema mpaka sasa kuna mgombea mmoja ambaye ni Rais aliyepo madarakani, Dk Ali Mohammed Shein, ambaye alichukua fomu na amesharudisha.
Kwa mujibu wa Vuai, Kamati hiyo itapendekeza jina litakalopelekwa kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na baadaye jina hilo litaenda mbele ya kikao cha NEC kitakachofanya uamuzi wa mwisho.
“Kwa mujibu wa Ibara ya 114 (b) Kamati hiyo pamoja na kazi nyingine, ina kazi ya kufikiria na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, juu ya wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar, ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,” alisema Vuai.
Wajumbe wa Kamati hiyo Maalumu kwa mujibu wa Ibara ya 113, ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM na Makamu wa Rais wa Zanzibar anayetokana na CCM.
Wengine ni wajumbe wa Kamati Kuu ya NEC wanaotoka Zanzibar, wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Zanzibar, Makatibu wa CCM wa Mikoa ya Zanzibar na wajumbe wote wa NEC Taifa wanaotoka Zanziba
Continue Reading...

NYUMBA YA MWANAMUZIKI LADY JAY DEE YAPIGWA MNADA.

Kampuni ya udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers inapiga mnada wa nyumba ya mwanamuziki nyota wa bongo fleva, Lady Jay Dee, baada ya kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana katika moja ya magazeti ya kila siku, mnada huo utafanyika saa 5:00 asubuhi kwenye eneo la kiwanja hicho lililopo Mivumoni.
“Kwa idhini tuliyopewa na EFC Tanzania Limited tutauza kwa mnada wa hadhara, dhamana/nyumba ya mdaiwa wa benki hiyo,” linasema tangazo hilo.
“Mnada utafanyika tarehe 4/07/2015. Jina la mdaiwa/mdhamini- Judith Wambura Habash, dhamana.nyumba itakayouzwa-Kiwanja Plot No. 54BLK4, Mivumoni Kinondoni Dar es salaam, tarehe ya mnada-4/07/2015 kuanzia saa 5:00 asubuhi na kuendelea,” linaongeza tangazo hilo.
Juhudi za kumpata mwimbaji huyo wa kibao cha “Machozi” hakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo, lakini Gadner Habash ambaye alikuwa na uhusiano na Jay Dee na ambaye jina lake limeandikwa kwenye tangazo hilo kama jina la tatu la mwanamuziki huyo, alisema hana taarifa hizo, hali kadhalika meneja wake.
Habari kutoka ndani ya taasisi hiyo zinasema kuwa mwanamuziki huyo alisitisha ghafla kulipa deni lake Juni mwaka jana bila taarifa yoyote na hata alipokuwa akitafutwa, hakuwa anapokea simu.
Kwa mujibu wa afisa kutoka kampuni ya MEM, nyumba hiyo iliyotumika kama dhamana ya mkopo, ipo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa kilometa 901 za mraba, Tegeta Wazo na kina thamani ya Sh40 milioni.
Continue Reading...

ZITO AWATAJA WATUUMIWA WA MABILIONI USWISI.

Dar es Salaam. Kiongozi mkuu wa chama chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe jana alianika orodha ya majina ya watu wanaotuhumiwa kuhodhi akaunti zenye mabilioni ya fedha nje ya nchi, lakini akasita kuyataja kutokana na sababu za kisheria.
Zitto aliwapa waandishi wa habari orodha hiyo akisema waende kufanyia kazi kwa kuwahoji wahusika kulingana na taaluma yao.
Orodha hiyo ina majina yenye asili ya kiasia isipokuwa wachache ambao wanaonekana wana majina ya kibantu.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mwembeyanga, Temeke, Dar es Salaam, Zitto alisema: “Majina ninayo haya hapa niwataje nisiwatajee! Ni wengi sana wengine wanamiliki kampuni kubwa.”
Alisema Zitto alisema wamejaribu kuishinikiza Serikali ichukue hatua, lakini inaonekana kutotaka kufanya hivyo na kwamba anaamini waandishi wa habari kwa kutumia taaluma yao wataweza kuwaanika wahusika.
Wakati maofisa wa ACT wakigawa orodha ya majina hayo, wananchi walionekana kuwa na shauku ya kupata nakala ya karatasi hiyo yenye majina 99 ya wafanyabiashara hao maarufu ndani na nje ya nchi, lakini kiongozi huyo hakuwa tayari kuwapatia na badala yake akiwaambia wasome magazeti ya kesho (leo).
Zitto alisema kwamba kati ya majina ya raia hao wenye mabilioni ya fedha nchini Uswisi, kuna wengine wanamiliki kihalali lakini wengine wamejirundikia isivyo halali.
‘’Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo kwa Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo. Kila mwandishi wa habari aliyepo kwenye mkutano huu nimempatia nakala yenye majina 99 ya Watanzania au watu wenye uhusiano na Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswisi. Jumla ya akiba katika akaunti benki hii pekee ni Dola 114 milioni za Marekani,’’ alisema.
Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ametawazwa kuwa chifu wa mkoa na wazee wa Dar es Salaam na kuitaka serikali kuhakikisha inawarudishia wananchi chenji zinazotokana na ufisadi wa Escrow , EPA na Richmond. Akizungumza katika kongamano hilo la wazee la kutafakari uchaguzi wa mwaka 2015, Dk Slaa alisema ingawa wazee waliungana na Hayati Mwalimu Nyerere kupambana na maadui wa tatu ambao ni ujinga, umaskini na maradhi lakini kwa sasa ameongezeka adui wa nne ambaye ni ufisadi.
“Ujinga alioupinga Mwalimu na wazee umeondoka? Lakini ujinga, umaskini na maradhi na kuna adui wa nne ambaye ni ufisadi,” alisema.
Alisema hakuna Mtanzania ambaye atakwenda dukani na Sh10,000 kununua chumvi na kibiriti halafu akaacha chenji yake dukani kwa makusudi na hivyo Watanzania bado wanadai fedha zao zilizopotea kutokana na ufisadi.
Kadhalika Dk Slaa alisema kitendo cha wazee hao kukutana katika kongamano hilo kinaashiria kuwa wana kiu, njaa na matumaini ya kutaka mabadiliko.
Continue Reading...

AZAM TV KUONYESHALIGI YA UINGEREZA KWA KISWAHILI.

AZAM TV
uongozi wa azam media ukiwa na rais Jakaya Kikwete wakati wa ufunguzi wa studio mpya wa azam media.

Mambo yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili.
Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo live kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.
“Tunafanya juhudi kubwa ili tulifanikishe hilo mapema, ila wahusika ndiyo wenye uamuzi wa mwisho katika kutupa haki ya matangazo hayo, tumedhamiria pia kuonyesha Ligi ya Hispania.
“Wakati tukipanga haya, tuna nia ya kuboresha muonekano wa ligi yetu ya Tanzania (Ligi Kuu Bara) msimu ujao ambapo tunataka ionekane katika ubora wa hali ya juu zaidi,” alisema Tido.
Katika hatua nyingine, Tido alisema katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi hadi utakapofanyika, watakuwa wakiwaletea watazamaji wao matangazo ya matukio mengi kuhusu uchaguzi huo.
Continue Reading...

Saturday, July 4, 2015

KAMPENI YA MEDIA CAR WASH FOR CANCER YAFANYIKA DAR.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadick akizindua kampeni ya kuosha Magari katika viwanja vya Leaders Club kwa ajili ya kuchangia Fedha kwa waandishi wa Habari ambao wanamatatizo ya Kiafya ikiwemo Saratani ( MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),Nd.Assah Mwambene akikabidhi kiasi cha fedha kwa Mmoja wa Waratibu wa kampeni ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER Bw.Benjamin Thomson,zilizochangwa na Idara hiyo kupitia chama chao cha Maofisa Habari wa Serikali ,walijitolea kuchanga kiasi cha shilingi 1,680,000=.
Pichani kati anaeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda

Kama vile haitoshi nayo Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na michezo pia walifanikisha kuchangia kiasi cha shilingi 1,350,000/= kufuatia kuguswa kwa namna moja nyingine kwa kampeni  hiyo adhimu ya kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani.

Mbali ya fedha hizo kupatikana pia walijitokeza watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo ya MEDIA CAR WASH FOR CANCER,ambalo kwa kiasi kikubwa bado linahitaji kuongeza hamasa zaidi ili wadau wazidi kujitokeza na kuchangia.

Kampeni hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo na wadau wa habari walishiriki zoezi la kuosha magari kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha,huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam Mh said Meck  Sadick.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiendelea Kuosha moja ya Magari yaliyofika kuoshwa katika MEDIA CAR WASH FOR CANCER. Ikiwa ni kuchangia waandishi wa habari wenye magonjwa mbalimbali ikiwemo Saratani.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiosha Gari wakati wa  Shughuli hiyo maalum kwa ajili ya Kuchangia waandishi wenye udhoofu wa afya zao (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
Issa Michuzi wa Libeneke la Michuzi Blog na Michuzi Media Group akitimiza majukumu... Anaosha Moja ya Magari kwa ajili ya kuchangia waandishi wa habari ambao wana maradhi ya Saratani mapema leo kwenye kampeni.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO,Assah Mwambene akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Paul Makonda mara baada ya kushiriki zoezi zima la kuwachangia waandishi wa Habari wenye Matatizo mbalimbali yakiwemo na ya Saratani (MEDIA CAR WASH FOR CANCER).
 Picha ya pamoja ya waandishi wa Habari pamoja na Baadhi ya Viongozi 
Continue Reading...

DIAMOND AENDELEA KUNG'ARA. ACHAGULIWA KUWANIA TUZO UGANDA.

Diamond Platnumz ameendelea kutajwa kuwania tuzo mbalimbali barani Afrika, akiwa ni miongoni mwa wanaowania tuzo za MAMA zitakazotolewa mwezi huu, muimbaji huyo wa ‘Nana’ ametajwa kuwania tuzo zingine za Uganda zijulikanazo kama Uganda Entertainment Awards 2015 (UEA)
UEA-2
Platnumz anawania kipengele cha Best African Act akichuana na Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Tiwa Savage (Nigeria) na Active
UEA-1
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Septemba 4, 2015 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort (Speke Ball) jijini Kampala, Uganda.

Continue Reading...

USAILI WA BSS WAFANYIKA JIJINI MWANZA.

Majaji wa shindano la bss 2015 wakiwa kwenye usaili jijini mwanza
Pazia la shindano la kuimba Bongo Star Search mwaka 2015, limeanza rasmi leo mkoani Mwanza ambapo usaili umefanyika kwenye hoteli inayojulikana kama Lakairo.
Shindano hilo linaloibua vipaji vya vijana mwaka huu lina kauli mbiu mpya ya ‘Kuwa Original Chagua Original’ ambayo inawahimiza vijana kujitokeza na kuonesha vipaji vyao.
washiriki wa bss 2015 jijini mwanza wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye usaili.
Shindano hilo la kusaka vipaji vya kuimba kwa mwaka linatafanya usaili mikoa 5 ambapo Mwanza July 4-5 ndani ya ukumbi wa La kairo, July 11-12 Arusha ukumbi wa Triple 7, Mbeya ukumbi wa Club vibes July 18-19 na Dar July 24-26

Continue Reading...

Followers

Follow The Author