Katibu Mkuu Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto),
akizungumza wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati
ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka
Wizara ya Ulinzi nchini Urusi.Kikao hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano
wa wizara, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi
ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao
cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti
uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti
uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi nchini
Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es
Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa
maelezo kuhusu mada inayohusiana na
udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati
wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati
ya Tanzania na Urusi.Kushoto ni Kamishna
Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika
ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha
karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa
kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao
hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar
es Salaam
Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la
Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi
nchini Urusi, namna ya kudhibiti uhalifu
katika majengo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati
ya nchi hizo. Kikao hicho kilifanyika
leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
HABARI KWA HISANI YA LKITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI