Thursday, December 8, 2016

SERIKALI SASA YATAMBUA RASMI MITANDAO YA KIJAMII KUWA CHOMBO CHA HABARI.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akihutubia wakati wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa TBN, Joachim Mushi.

 Mmoja kati ya wamiliki wa mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo, akitoa moja ya somo katika mafunzo hayo.

 Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
 Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano,mafunzo hayo.
Picha ya pamoja. Picha zote na Mafoto Blog
 Mmiliki wa Blog hii, Sufianimafoto akifuatilia kilichokuwa kikiendelea ukumbini hapo.
 Blogger Kitime akichangia mada
Maofisa wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NMB wakibadilishana mawazo. Kushoto ni Doris na Joyce Nsekela. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Continue Reading...

Thursday, October 27, 2016

KAMPUNI YA YARA TANZANIA YAZINDUA RASMI USAFIRISHAJI WA MBOLEA KWA NJIA YA TRENI


 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL, Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani.

 Azungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alisema kuwa YARA kwa kushirikiana na TRL na SAGCOT, wameamua kuzindua njia hiyo ya usafirishaji ili kupunguza gharama za usafirishaji kwa kutumia barabara na maji ili kuwafikia walengwa kwa wakati na kwa gharama nafuu, ambapo awali kusafirisha Tani moja kutoka Viwandani Ulaya hadi jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni Dola za Kimarekani 40, kwa Tani moja na Dar es Salaam hadi Tabora ni Dola za Kimarekani 100 kwa Tani moja kwa njia ya barabara. 

Aidha  Macedo, alisema kuwa kuamua kutumia usafiri wa Treni sasa usafiri utashuka kwa asilimia 35.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo, kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo (wa pili kulia) na Afisa Habari wa YARA Tanzania, Lynda Byaba (kulia), kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Mafoto Blog
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali ya Ofisi kwao wakati walipotembelea kwenye uzinduzi wa usafirishaji kwa njia ya Treni uliofanyika leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akionyesha jinsi mbolea inavyopakiliwa kwenye Mabehewa kabla ya kusafirishwa.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.

Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.
 Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.
 Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.
 Mifuko ya Mbolea ikiwa tayari kupakiwa kwenya magari ili kusogezwa eneo la kupakilia kwenye Mabehewa ya Treni
 Wafanyakazi wa YARA wakijiandaa kushusha katika magari na kupakia kwenye Mabehewa.
 Mabehewa yakisubiri kupakiliwa.....
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari waliotembelea Ofisi hizo leo wakati wa uzinduzi huo.
Continue Reading...

Friday, October 7, 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NJE JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje  Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia njia za mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Mjumbe  kutoka  Jeshi la Polisi,Kamishna  Albert Nyamhanga akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya  Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo  yalifanyika jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

 Naibu Waziri wa  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto),  baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu  za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek Mazungumzo  yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.(Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Continue Reading...

Saturday, September 3, 2016

TANZANIA URUSI ZABADALISHANA UZOEFU WA KUDHIBITI UHALIFU



                    Katibu Mkuu  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kushoto), akizungumza wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao  hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.

      Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira ( kushoto), akiangalia video inayoonyesha jinsi ya kudhibiti uhalifu wa barabarani kwa kutumia kamera maalum, wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kulia ni wataalamu wa masuala ya kudhibiti uhalifu kutoka Wizara ya Ulinzi  nchini Urusi.Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.

            Mtaalamu wa mifumo ya Komputa , Boris Derygin akitoa maelezo kuhusu  mada inayohusiana na udhibiti wa uhalifu wa mitandao wakati wa kikao  cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi.Kushoto  ni Kamishna Msaidizi wa Polisi, SACP Gabriel Mukungu. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, Dar es Salaam.

         Mtaalamu wa mifumo ya Komputa, Boris Derygin ,akionyesha karatasi inayoelekeza jinsi ya kuitambua gari iliyofanya uhalifu wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya Tanzania na Urusi. Kikao hicho kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam

               Kamishna Msaidizi , SACP Gabriel Mukungu wa Jeshi la Polisi la Tanzania, akielekezwa na Kapteni Vasily Gerasimov wa Wizara ya Ulinzi nchini Urusi, namna  ya kudhibiti uhalifu katika majengo wakati wa kikao cha  kubadilishana uzoefu wa kudhibiti uhalifu kati ya nchi hizo. Kikao hicho  kilifanyika leo katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

HABARI KWA HISANI YA LKITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Continue Reading...

Wednesday, August 31, 2016

SIRI UNAYOTAKIWA KUIJUA WEWE MKE AU MUME, by Dr Chris Mauki (phd in psychology)

msaidie
(Mentor wangu Myles Munroe RIP alinisaidia kitu, nadhani nikiweka mkazo kitakusaidia na wewe)
Yako mambo ambayo ni muhimu kukumbuka katika suala zima la kutoa na kupokea baina ya mume na mke katika ndoa. Mwanaume anapoonyesha kutaka au kuhitaji kitu kutoka kwa mwanamke, mwanamke huhamaki, wakati mwanaume akitoa kitu kumpa mwanamke, mwanamke huitika kwa hujisogeza karibu na mwanaume (hapa namaanisha kuwa mwanamke anapopokea kitu kutoka kwa mwanaume yeye hujikuta anaongeza kuwa karibu zaidi na mwanaume huyu kuliko wakati ambao mwanamke ndiye anayempa kitu mwanaume). Katika asili hii utaona uhalisi wa mwanaume kumtimizia mahitaji mwanamke na sio mwanamke kumtimizia au kumtunza mwanaume (ni jambo la asili mwanaume kumpa mahitaji mwanamke na sio mwanamke kumpa mahitaji mwanaume). Mwanaume anapojitoa kwa moyo kwa ajili ya mwanamke, mwanamke kunyenyekea bila shuruti. Hakuna kilicho cha thamani sana kwa mwanamke zaidi ya mwanaume mwenye uwezo wa kujitoa kwa moyo wa dhati kwa ajili ya mke wake. Hakuna kinacho muumiza na kumkatisha tamaa mwanamke kama kuwa na mwanaume asiyeweza kujitoa kwa moyo wa dhati kwa ajili ya mke wake. Ngoja nikushirikishe siri iliyopo hapa; Kama unatamani kuwa na mwanamke mnyenyekevu basi jifunze kujitoa kwa moyo wa dhati kwake, unapoonyesha kutaka kumuumiza mkeo, mkeo naye kuonyesha kujihami au kukukwepa. Pale mwanaume anapomshirikisha mwanamke na mwanamke naye huongeza kumjali mwanaume. Mwanaume anapoonyesha kuongoza, kwa uongozi wenye uwajibikaji, basi na mwanamke naye huonyesha kufuata uongozi ule. Uongozi hapa simaanishi kuwa bosi wa mkeo, kila siku unatoa amri za nini unataka kifanywe na kifanywe vipi, la hasha, kwa kuwa kiongozi hapa namaanisha kutangulia mbele na kuwaonyesha wengine njia, sio wewe kuwaweka wengine mbele wakati wewe unakwepa au unahofia hatari. Kuongoza hapa namaanisha kumwonyesha mwenza wako namna bora ya kufanya au namna bora ya kuenenda. Ukisema hutaki kitu fulani basi unaonyesha kwa vitendo nini unachokitaka na kwanamna gani unakitaka kiwe au kifanywe. Hapa namaanisha kuongoza kwa mifano (leading by examples). Ukiwachunguza viongozi wote wa kwenye vitabu vitakatifu, iwe Biblia au hata Quran, utagundua kwamba wote waliongoza kwa mifano. Fahamu hili na ulizingatie litakusaidia sana.
Continue Reading...

MASAUNI AZINDUA PROGRAMU YA “TUNZA AMANI IKUTUNZE” JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO) , Kulia ni Mkurugenzi wa shirika hilo, Askofu Nason Ngoy Ngoy. Hafla hiyo imefanyika   leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.


 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza mara baada ya uzinduzi wa  Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO). Hafla hiyo imefanyika  leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam

             Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC), Dk. Hellen Kijo Bisimba akizungumza mara baada ya uzinduzi wa  Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, wakati wa uzinduzi wa mkakati huo wenye lengo la kudumisha amani ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO). Hafla hiyo imefanyika  leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.

                 Mkurugenzi wa Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania (PSEDO).  Askofu Nason Ngoy Ngoy, akizungumza wakati wa  uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE. Hafla hiyo imefanyika  leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam.

               Washiriki wa uzinduzi wa Kitabu, DVD na CD zenye ujumbe wa “TUNZA AMANI IKUTUNZE”, ulioratibiwa na Shirika la Kukuza Amani na Uchumi Tanzania(PSEDO), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam

Continue Reading...

Thursday, January 14, 2016

DARASA LA SAIKOLOJIA NA DR CHRIS MAUKI: TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA AU WENYE MAZINGIRA YA KUJA KUFANIKIWA

Dr Chris Mauki

Kufanikiwa ni kiu ya kila mmoja ingawa ukweli ni kwamba wengi wetu tunabaki tunayatamani mafanikio wakati hatuna mazingira yeyote ya kuruhusu mafanikio hayo yawepo au yatujie. Hapa nakuletea tabia za watu wawili tofauti, mmoja akiwa ni mtu mwenye mafanikio au yule ambaye ana mazingira ya kuja kufanikiwa na mwingine ni mtu asiye na mafanikio na asiye na mazingira ya kufanikiwa maishani. Nitaanza na tabia za watu wenye mafanikio;
1. Ni watu wenye kushukuru kwa kila jambo, sio wenye kutoa lawama2. Ni watu wenye tabia ya kupongeza pale wanapoona mwingine anastahili pongezi3. Ni watu wenye tabia ya kusamehe, tena wanasamehe kwa urahisi wala sio kwa kuombwa na kulazimishwa4. Ni watu wasioona uchungu kuwapongeza wengine au kukubali wengine wanapopata ushindi wa aina yeyote, na sio tu kuwapongeza bali pia hawaoni ugumu kuwasaidia au kuwashauri wengine ili wafanikiwe zaidi5. Ni watu wanaokubali wakati wote kubeba majukumu au lawama pale wanaposhindwa kufanya inavyopaswa, sio wenye kujitetea au kujaribu kukwepa majukumu6. Ni watu wenye tabia ya kupenda kusoma kitu kila siku, sio wavivu wa kusoma au kutafuta taarifa na ujuzi7. Ni watu wenye tabia ya kuweka utaratibu wa nini kinafanyila leo na nini kitafanyika kesho na kwa nini kifanyike, sio watu wanaoburuzwa na mazingira yanaowazunguka au kuendeshwa na marafiki zao8. Sio watu wenye kuzungumza sana kuhusu watu wengine na madhaifu yaw engine bali ni wenye kuzungumza zaidi kuhusu mawazo ya kujenga au mawazo ya kimaendeleo9. Mara zote wana kiu ya kuona wengine wanafanikiwa, hata kama mafanikio hayo yatayazidi yale wao walionayo10. Sio wachoyo katika kutoa taarifa au ujumbe wowote muhimu kwa mtu yeyote, maana wao hawana uchungu na mafanikio au ushindi wa mwingine11. Ni watu wenye kuonyesha furaha wakati wote, sio wenye kununa, kuzira na kuwa na huzuni mara kwa mara12. Ni watu wanaoweka malengo na kuongozwa na malengo katika maisha yao ya kila siku, sio wanaokurupuka kufanya mambo kwa hisia, misukumo au mashindano tu13. Sio waoga wa mabadiliko, bali hutamani mabadiliko chanya na yenye kujenga na kuleta maendeleo, na kwahiyo mara zote kuyawezesha mabadiliko kutokea kwao na kwenye maisha ya wengine na sio kuyapinga14. Kwao kujifunza ni tabia endelevu sio jambo linalotokea wakati wakiwa shuleni tu, wao huhesabu maisha ya kila siku ni kama shule15. Kiu na msukumo wa maisha yao ya kila siku ni katika kusababisha mabadiliko, aidha mabadiliko kwao wao binafsi au kwa wale wanaowazunguka.
Continue Reading...

Followers

Follow The Author